Pembetatu ya Kiangazi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Pembetatu ya Kianganzi)
Pembetatu ya Kiangazi (Summer Triangle) jinsi inavyoonekana Tanzania

Pembetatu ya Kianganzi (ing. summer triangle) ni umbo la pembetatu kwenye anga la nusutufe ya kaskazini ya Dunia inayofanywa na nyota angavu tatu ambazo ni Vega katika Kinubi (Lyra), Dhanabu ya Ukabu (Deneb) katika Dajaja (Cygnus) na Tairi (Altair) katika Ukabu (Aquila).

Pembetatu ya Kiangazi si kundinyota halisi jinsi zinavyoelezwa na Ukia, bali nyota zake ni sehemu za makundinyota matatu tofauti za Kinubi (Lyra), Dajaja (Cygnus) na Ukabu (Aquila).

Usiku wa manane pembetatu hii inaonekana vema katikati ya anga katika nchi za nusutufe ya kaskazini wakati wa Juni - Agosti. Katika Afrika ya Mashariki inafika tu kiasi juu ya upeo wa anga kuanzia masaa ya jioni hadi usiku manane katika miezi ya Agosti hadi Novemba.

Nyota za Pembetatu[hariri | hariri chanzo]

Jina Kundinyota Mwangaza unaoonekana Mwangaza halisi
(× solar)
Spectral type Umbali
(miakanuru)
Rediasi
(x rediasi ya Jua)
Vega Kinubi (Lyra) 0.03 52 A0 25 2.36 - 2.82
Dhanabu ya Ukabu (Deneb) Dajaja (Cygnus) 1.25 70000 A2 3550 203 ± 17
Tairi (Altair) Ukabu (Aquila) 0.77 10 A7 16.6 1.63 - 2.03