Nenda kwa yaliyomo

Pembetatu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Pembetatu ni umbo bapa lenye pande tatu zisizonyoka na kukutana kwenye pembe tatu za kila kona.

Jumla ya kiwango cha pembe zote tatu ni nyuzi 180. Eneo la pembetatu ni nusu kitako mara kimo.

Pembe zatajwa kwa kawaida kwa herufi za kwanza katika alfabeti ya Kigiriki yaani alfa, beta na gamma.

Elimu inayoshughulia pembetatu ni jiometria na hsasa tawi la trigonometria.

Aina za pembetatu

[hariri | hariri chanzo]

Pembetatu hupangwa kufuatana na tabia za pande zao:

  • Kwenye pembetatu pandesawa pande zote tatu ni sawa.
  • Kwenye pembetatu pacha pande mbili ni sawa.
  • Kwenye pembetatu mshato (= pia pembetatu guni) pande zote ni tofauti.
Pembetatu pandesawa Pembetatu pacha Pembetatu mshato
pandesawapachamshato

Pembetatu hupangwa pia kufuatana na tabia za pembe zao:

  • Pembetatu mraba ina pembe moja ya 90°.
  • Pembetatu butu ina pembe moja ambayo ni kubwa ya 90°.
  • Pembetatu kali ina pembe ambazo zote ni ndogo kuliko 90°.
  • Pembetatu mshazari ni kila pembetatu isiyo mraba.
Right triangle Obtuse triangle Acute triangle
mrababutukali
 
 mshazari
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Pembetatu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.