Nenda kwa yaliyomo

Peek Freans

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Peek Freans ni aina ya chakula ya biskuti au vitafunio. Aina hii inamilikiwa na United Biscuits (katika Uingereza) ingawa jina la "Peek Frean" halitumiki tena Uingereza. Katika Marekani na Kanada, Peek Freans inamilikiwa na Kraft Foods.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Peek, Frean na Wenzake ilianzishwa katika mwaka wa 1857 katika eneo la Bermondsey, London, Uingereza na waanzilishi James Peek na George Hender Frean. Katika mwaka wa 1861, kampuni hii ilianza kusafirisha biskuti ili ziuzwe nchini Australia na ,baadaye,katika maeneo mengine ya ng'ambo. Walihamia kiwanda kubwa zaidi katika Bermondsey katika mwaka wa 1866 walipoendelea kuoka biskuti hizo mpaka zilipoachishwa katika mwaka wa 1989.

Katika mwaka wa 1861, walianzisha biskuti ya Garibaldi. Katika mwaka wa 1910, kampuni ilianzisha biskuti zake za kwanza za cream, hivi sasa zinajulikana kama biskuti za aina ya Bourbon.Katika mwaka wa 1924, walijenga kiwanda chao cha kwanza nje ya Uingereza , kiwanda kilijengwa Dum Dum, Uhindi.

Katika mwaka wa 1921, Peek Frean iliingia katika mkataba na kampuni shindani ya Huntley & Palmers. Mkataba huu ulisababisha kuundwa kwa kampuni ya kutayarisha biskuti ya Associated Biscuit Manufacturers. Hata hivyo, kampuni zote mbili ziliendesha majina ya bidhaa zao na maeneo yao ya kazi.

Mwaka wa 1949 ulishuhudia kuanzishwa kwa jumba la kwanza la kampuni la uokaji knchini Kanada. Jumba hilo la uokaji , linalopatikana katika barabara ya Bermondsey Road katika East York, Ontario, bado linazalisha bidhaa.

Katika maisha ya kampuni hiyo, ilibadilisha jina lake kutoka Peek, Frean na Wenzake hadi likawa Peek Frean(katika mwanzo wa karne ya ishirini) na kisha Peek Freans(katika miaka ya 1970). Jina hilo likatumika sana katika bidhaa zake kwa miaka mingi.

Angalia Pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
  1. Peek Frean's Biscuit Factory in Bermonsey, London
  2. Biscuit Factory Makes 'Comeback', BBC News, 8 Feb 2005 [2]