Nenda kwa yaliyomo

Paul Erman

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Paul Erman.

Paulo Erman (29 Februari 1764 - 11 Oktoba 1851) alikuwa mwanafizikia kutoka Berlin nchini Ujerumani.

Babake Jean Pierre Erman (1735-1814) alikuwa mwanahistoria, mwanatheolojia na mhubiri kwenye kanisa la Waprotestanti Wafaransa mjini Berlin.

Erman alikuwa mwalimu wa sayansi kwa ufanisi katika shule ya sekondari ya Kifaransa huko Berlin. Alihamia kufundisha kwenye chuo cha kijeshi, na miezi 18 baadaye alichaguliwa kuwa profesa wa fizikia wa chuo hicho.

Kazi yake ilikuwa inahusiana na umeme pamoja na sumaku, ingawa pia alitoa michango katika elimumaonzi na Fiziolojia.

Erman alikufa Berlin. Aliacha mwanae, Georg Adolf Erman ambaye alikuwa mwanafizikia, na mjukuu Johann Peter Adolf Erman anayejulikana kama mtaalamu wa nchi ya Misri (Egyptologist).

Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Paul Erman kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.