Paul Allen

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Paul Allen

Paul Gardner Allen (Januari 21, 1953 - Oktoba 15, 2018) alikuwa mfanyabiashara mkubwa wa Marekani, muundaji wa programu za kompyuta, mtafiti, mwekezaji, na mfadhili. Alianzisha kampuni ya "Microsoft Corporation" na rafiki yake wa utotoni Bill Gates mnamo 1975, ambayo ilisaidia kuibua mapinduzi ya kompyuta ndogo miaka ya 1970 na 1980.

Microsoft ikawa kampuni kubwa zaidi ya programu za kompyuta binafsi ulimwenguni..[1] Allen aliorodheshwa kama mtu tajiri zaidi wa 44 ulimwenguni na gazeti la Forbes mnamo 2018, na wastani wa utajiri wa dola za kimarekani bilioni 20.3 wakati wa kifo chake.[2][3]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

People.svg Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Paul Allen kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.