Patience Okon George

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Patience Okon George (alizaliwa 25 Novemba 1991) ni mwanariadha wa Nigeria.[1][2] Alishiriki katika mashindano ya mita 400 katika Mashindano ya Dunia ya Riadha ya 2015 huko Beijing, Uchina[3] na pia katika michezo ya Olimpiki ya Rio ya 2016. George ni mshindi mara mbili wa medali ya shaba katika mashindano ya Afrika ya mbio za mita 400. Yeye pia ni bingwa wa kitaifa wa Nigeria mara tatu katika mbio za mita 400.[4]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Rio 2016 Bio.". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-11-25. Iliwekwa mnamo 2021-10-30. 
  2. "Patience Okon GEORGE | Profile | World Athletics". www.worldathletics.org. Iliwekwa mnamo 2021-10-30. 
  3. Haets Results
  4. Tunde Eludini. "Ogunlewe, Okon win third national titles at 2017 All-Nigeria Championships – AthleticsAfrica". www.athletics.africa (kwa en-GB). Iliwekwa mnamo 2021-10-30.