Oresund

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Oresund inavyoonekana kutoka upande wa Uswidi

Oresund (Kidenmark: Øresund, Kiswidi: Öresund) ni mlangobahari unaotenganisha kisiwa cha Zealand (Sjælland) katika Denmark na jimbo la Skone (Skåne) katika Uswidi.

Oresund ni moja kati ya milango mitatu ya bahari inayopita katika visiwa vya Denmark na kuunganisha Bahari ya Kaskazini na Bahari ya Baltiki kwa njia ya Kattegat na Skagerak. Ni kati ya njia za bahari duniani zenye meli nyingi sana.

Tangu mwaka 2000 kuna daraja la kuvukia Oresund kutoka Denmark kwenda Uswidi. Lilifunguliwa rasmi tarehe 1 Julai mwaka 2000 na mfalme Carl XVI Gustav wa Uswidi na malkia Margrethe II wa Denmark.

Viungi vya nje.[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Oresund kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.