Oleksandr Zinchenko

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Faili:Zinch 2018.jpg
Oleksandr Zinchenko

Oleksandr Zinchenko (alizaliwa 15 Desemba 1996) ni mchezaji wa Ukraina ambaye anacheza kama kiungo mshambuliaji wa klabu ya Ligi Kuu ya Uingereza iitwayo arsenal na timu ya taifa ya Ukraine.

Kazi ya Klabu[hariri | hariri chanzo]

Zinchenko alianza kazi yake katika klabu ya Ligi ya Urusi ya FC Ufa kabla ya kujiunga na klabu ya Manchester City mwaka 2016 kwa ada ya £ 1 milioni.Anacheza kama Kiungo wa kati, pia anaweza kucheza katika nafasi nyingi kama beki wa kushoto.

Kazi ya kimataifa[hariri | hariri chanzo]

Alicheza mechi yake ya kimataifa katika mechi ya kufuzu ya UEFA Euro mwaka 2016 dhidi ya Hispania.Zinchenko alifunga goli lake la kwanza la kimataifa katika mechi ya kirafiki dhidi ya majirani zao Romania huko Turin, ambapo Ukraine ilishinda 4-3 tarehe 29 Mei 2016.

Pia akawa mchezaji mdogo kuliko wa timu ya taifa ya Ukraine na mchezaji mdogo wa kwanza kufunga goli la kimataifa wakati akiwa na umri wa miaka 19,akivunja rekodi ya Andriy Shevchenko.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Oleksandr Zinchenko kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.