Nenda kwa yaliyomo

Ofisi ya kamishna mkuu wa haki za binadamu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ofisi ya kamishna mkuu wa haki za binadamu (kifupi: OHCHR) ni idara au kitengo cha sekretarieti ya Umoja wa Mataifa inayotenda kazi ya kukuza na kulinda haki za binadamu ambazo zinasimamiwa chini ya sheria za kimataifa na zilizoainishwa katika Azimio la Haki za Binadamu la mwaka 1948.

Ofisi iliundwa na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa uliofanyika tarehe 20 Disemba 1993[1] baada ya Mkutano wa Dunia wa Haki za Binadamu.[2]

Ofisi hiyo inaongozwa na Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu, anayeratibu shughuli za haki za binadamu katika Mfumo mzima wa umoja wa mataifa na hukaimu kama sekretarieti wa Baraza la Haki za Binadamu mjini Geneva nchini Uswisi. Kamishna Mkuu wa sasa ni Michelle Bachelet wa nchini Chile, ambaye alichukua nafasi ya Zeid Raad Al Hussein wa nchini Jordan mnamo tarehe 1 Septemba 2018.[3]

Miaka 2018–2019, idara ilikuwa na bajeti ya dola za Kimarekani milioni 200.6 sawa na asilimia 3.7 ya bajeti ya kawaida ya umoja wa mataaifa,[4] na takriban wafanyikazi 1,300 walioko Geneva na mji wa New York. Ni mshiriki wa zamani wa Kamati ya Kikundi cha Maendeleo cha Umoja wa Mataifa.

  1. "OHCHR | Brief history". www.ohchr.org. Iliwekwa mnamo 2020-01-25.
  2. "Brief history". Iliwekwa mnamo 5 Septemba 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "OHCHR | High Commissioner - Michelle Bachelet Jeria". www.ohchr.org. Iliwekwa mnamo 2020-01-25.
  4. "OHCHR | Funding and Budget". www.ohchr.org. Iliwekwa mnamo 2020-01-25.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]