Obby One
Makala hii inahusu mada au mtu asiyejulikana sana. Kuna mashaka kama mada inastahili kuwa na makala katika kamusi. Onyo hili linaweza kuwekwa pia kama makala haionyeshi umaarufu, hata kama upo.
Watumiaji wanaombwa kushiriki katika majadiliano kama makala hii inafaa kubaki au la. Tazama:Wikipedia:Umaarufu
Unaweza kuondoa kigezo hiki kama majadiliano yametokea na washiriki walipatana.
Wilbard Richard Mmbando (anajulikana kwa jina la Obby One, alizaliwa Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro, 13 Aprili 1999) ni msanii, mwimbaji na mtunzi wa nyimbo kutoka Tanzania.
Obby One amepata mafanikio makubwa katika mauzo ya nyimbo zake kutoka na ubunifu alionao kwenye uandishi wa mashairi na namna anavyoyaimba Kwa miondoko ya Bongo Flava, R&B na Afrobeat.
Katika mahojiano Yake na kituo kimoja Cha redio jijini Dar es Salaam, Obby One alitaja kuwa Sugar, Bow Down pamoja Come Closer ndizo nyimbo zake pendwa zilizomuongezea mashabiki wengi na kumfanya ashiriki kufanya maonyesho mengi ya wazi ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.
Historia ya muziki
[hariri | hariri chanzo]Alianza muziki pindi tu alipo anza elimu yake ya sekondari katika shule ya sekondari Ritaliza mwaka 2014 ambapo alianza kuimba kwaya.
Aligundua ana kipaji pale alipokuwa na uwezo wa kukariri mashairi ya nyimbo zilizoimbwa na wasanii wengine ambazo zilimpa njia nzuri ya namna ya kuandika nyimbo zake mwenyewe.
Amejizolea umaarufu mkubwa Nchini Tanzania alipojiunga na elimu ya juu na amefanikiwa kupata Mashabiki wengi wanaopenda aina ya Muziki anaoufanya.
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Obby One kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |