Nenda kwa yaliyomo

Oaxaca (jimbo)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bendera ya Oaxaca
Mahali pa Oaxaca katika Mexiko

Oaxaca ([wɑˈhɑkə]; jina rasmi: Estado Libre y Soberano de Oaxaca; Kiswahili: dola huru na enzi ya Oaxaca) ni moja kati ya majimbo ya Mexiko upande wa jusini ya nchi, magharibi wa shingo ya nchi ya Tehuantepec. Mji mkuu na mji mkubwa ni Oaxaca. Imepakana na Guerrero, Puebla, Veracruz na Chiapas. Upande wa kusini ni maji ya Pasifiki.

Kunako mwaka wa 2005, idadi ya wakazi ilikuwa 3,506,821. Una eneo la 93,952 km².

Oaxaca ilikuwa sehemu ya maeneo ya Wazapotec na Wamixtec. Jina lake limetokana na jina la mji wa Oaxaca.

Gavana wa jimbo ni Ulises Ruiz Ortiz.

Lugha rasmi ni Kihispania.

Miji Mikubwa[hariri | hariri chanzo]

  1. Oaxaca (258,008)
  2. San Juan Bautista Tuxtepec (144,555)
  3. Salina Cruz (71,314)
  4. Juchitán de Zaragoza (70,714)

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Monte AlbanMakala hii kuhusu maeneo ya Mexiko bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Oaxaca (jimbo) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.