Nyumba ya wageni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha ya nyumba ya wageni

Nyumba ya wageni (pia "gesti" kutoka Kiing. guest house) ni jengo penye nafasi za kukodi kwa kulala wageni.

Ndani yake kuna sehemu ya mapokezi, vyumba vya kulala na nafasi za bafu. Mara nyingi huwa pia na sehemu ya kupata chakula au angalau vinywaji.

Aina za nyumba za wageni[hariri | hariri chanzo]

Kuna aina nyingi tofauti za nyumba za wageni. Zile zenye nafasi nzuri zinafanana na hoteli zikiwa na vyumba vyenye kitanda kimoja au viwili na bafu la pekee kwa kila chumba, mara nyingi pia simu na TV ya chumbani pamoja na huduma ya intaneti.

Kinyume chake kuna pia nyumba zenye nafasi za kimsingi kabisa kama vyumba vikubwa vyenye vitanda vingi, bafu na choo kimoja tu kwa wageni wote na kadhalika.

Kwa kawaida nyumba ya wageni ni ndogo kuliko hoteli na huwa na nafasi duni zaidi.

Hosteli[hariri | hariri chanzo]

Neno hosteli lamaanisha mara nyingi aina za nyumba ya wageni zilizojengwa hasa kwa ajili ya vijana. Kuna chama cha kimataifa cha hosteli za vijana; hosteli hizi zina nafasi za ulala kwa bei ndogo; katika nchi nyingi ni sharti kuwa na kadi ya uanachama kwa kulala hapa.

Neno Hostel atumiwa pia kwa malalo ya wanafunzi au wafanyakazi wa kiwanda wasio safarini.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Nyuma za wageni zimejulikana katika historia ya wanadamu tangu milenia. Nyumba ya wageni mashuhri sana ni ile ya Bethlehemu ambako Yosefu na Mariamu walikosa nafasi wakati wa kuzaliwa kwake Yesu. Kote ambako walianza kwenda safari za mbali haja ya kuwa na malalo ya kukodisha ilijitokeza.

Kati ya nyumba za wageni mashuhuri za historia ni karavansarai za Uajemi na nchi za Mashariki ya Kati zilizojengwa kwenye barabara kwa umbali wa mwendo wa siku 1; zilikuwa na nafasi za kupokea wasafiri pamoja na nyama zao n kuwapatia malalo na chakula. Shah Abbas I wa Uajemi hukumbukwa kwa kujenga zaidi ya karavansarai 400 nchini mwake.