Nyoka mabaka
Mandhari
Nyoka mabaka | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||
Spishi 4:
|
Nyoka mabaka ni nyoka wa jenasi Chamaelycus katika familia Lamprophiidae walio na mabaka mgongoni.
Nyoka hawa ni wafupi, hadi sm 37 lakini sm 20-34 kwa kawaida. Rangi ni kijivu au kahawia na wana mabaka meusi mgongoni.
Tabia za nyoka mabaka hazijulikani sana. Inaonekana kama hukiakia ardhini usiku. Hula wadudu na mayai ya reptilia lakini mijusi pia.
Nyoka hawa hawana sumu na kwa kisa chochote wako wadogo sana na hawawezi kung'ata watu.
Spishi
[hariri | hariri chanzo]- Chamaelycus christyi, Nyoka Mabaka wa Christy (Christy's banded snake)
- Chamaelycus fasciatus, Nyoka Mabaka Magharibi (Ituri banded snake)
- Chamaelycus parkeri, Nyoka Mabaka wa Parker (Parker's banded snake)
- Chamaelycus werneri, Nyoka Mabaka wa Werner (Werner's banded snake)
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nyoka mabaka kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |