Nusuranyota
Nusuranyota (kwa kiingereza: quasar) ni kiini angavu sana cha majarra hai. Nguvu ya mnururisho wake inatokana na shimo jeusi la tungamomno, lenye tungamo kutoka tungamo ya Jua milioni kumi hadi bilioni kumi, na huzingirwa na kisahani cha uongezekaji. Kuanguka kwa gesi ya kisahani hupasha joto na hutoa nishati yenye jinsi ya mnururisho sumakuumeme. Nishati ng’avu ya nusuranyota ni kubwa mno; nusuranyota zenye nguvu zaidi zina mng’aro maelfu ya mara mkubwa kuliko majarra kama Njia Nyeupe.[1][2] Nusuranyota huainizishwa kama kijamii cha jamii kubwa zaidi ya kiini cha majarra hai. Misogeo miekundu ya nusuranyota inatokana na kuvimba kwa Ulimwengu.[3]
Istilahi nusuranyota ni ambatani ya nusura na nyota. Kwa kiingereza, quasar ni mkato wa “quasi-stellar radio source”—kwa sababu zilitambuliwa kwanza wakati wa miaka ya 1950 kama violwa vya asili isiyojulikana ambavyo hutokeza mawimbiredio—na zilipochunguzwa kwa masafa wa mawimbi yanayoonekena, zilifanana na nukta dhaifu ya nuru kama nyota. Taswira za mwonekano wa juu za nyota, hasa kutoka Darubini ya Angani ya Hubble, zimeonyesha kwamba nusuranyota ziko katika vitovu vya majarra, na majarra nyingine zinaingiliana sana au zinachanganyana.[4]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Wu, Xue-Bing; na wenz. (2015). "An ultraluminous quasar with a twelve-billion-solar-mass black hole at redshift 6.30". Nature. 518 (7540): 512–515. arXiv:1502.07418. Bibcode:2015Natur.518..512W. doi:10.1038/nature14241. PMID 25719667. S2CID 4455954.
- ↑ Frank, Juhan; King, Andrew; Raine, Derek J. (Februari 2002). Accretion Power in Astrophysics (tol. la Third). Cambridge, UK: Cambridge University Press. Bibcode:2002apa..book.....F. ISBN 0521620538.
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Quasars and Active Galactic Nuclei". ned.ipac.caltech.edu. Iliwekwa mnamo 2020-08-31.
- ↑ Bahcall, J. N.; na wenz. (1997). "Hubble Space Telescope Images of a Sample of 20 Nearby Luminous Quasars". The Astrophysical Journal. 479 (2): 642–658. arXiv:astro-ph/9611163. Bibcode:1997ApJ...479..642B. doi:10.1086/303926. S2CID 15318893.
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nusuranyota kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |