Ntone Edjabe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kigezo:Tfm

Ntone Edjabe
Born1970
Douala, Cameroon
OccupationWriter, journalist, DJ
NationalityCameroon

Ntone Edjabe (alizaliwa mnamo mwaka 1970) ni mwandishi wa habari wa Kameruni, DJ na mhariri mwanzilishi wa jarida la Chimurenga.

Maisha na kazi[hariri | hariri chanzo]

Ntone Edjabe alizaliwa Douala, Kameruni, na alihamia Lagos, Nigeria, ambako alianza masomo yake. Mnamo mwaka 1993 alikatisha masomo yake na kuhamia inchini Afrika Kusini.[1] Alifanya kazi kama mwandishi wa habari, mwandishi, DJ, na mkufunzi wa mpira wa magongo.[2]

Mnamo mwaka 1997 alikua mwanzilishi mwenza na msimamizi wa Soko la Pan African, sehemu ya kibiashara na kiutamaduni iliyokuwa Mtaa wa Long Street(Cape Town) katikati mwa Cape Town. Mnamo mwaka [[2002] alianzisha jarida la "Chimurenga". Mnamo mwaka 2004 alikuwa msimamizi[3] wa Time of the Writer, na mnamo mwaka 2007 alishiriki katika toleo lake la 10 katika Kituo cha Sanaa za Ubunifu za Chuo Kikuu cha KwaZulu-Natal. Edjabe ni mwanzilishi mwenza na mwanachama wa mfumo wa pamoja wa DJ Fong Kong Bantu Soundsystem. Mnamo mwaka 2009 alikuwa Msanii wa Makazi ya Abramowitz Taasisi ya Teknolojia ya Massachusetts.[4]

Mnamo mwaka 2011 Edjabe alishinda Tuzo kuu ya Prince Claus Awards, na yake Chimurenga platform.

Kazi zake[hariri | hariri chanzo]

Mnamo mwaka 2002, Edjabe alikua mwanzilishi na mkurugenzi wa jarida la "Chimurenga" na msimamizi wa mfululizo wa machapisho African Cities Reader na Edgar Pieterse. Alishirikiana na kuwasilisha kipindi cha redio Soul Makossa cha Bush Radio (South Africa)|Bush Radio 89.5, redio iliyojikita huko Cape Town.[5] Alikuwa mtunzi akiwa na mwenzake Neo Muyanga wa Pan African Space Station (PASS). Miongoni mwa machapisho ambayo alichangia ni Politique africaine, Autre Afrique|L'Autre Afrique na BBC Focus on Africa.

Insha na makala[hariri | hariri chanzo]


Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. "The New South Africa with Ntone Edjabe" Archived 28 Septemba 2011 at the Wayback Machine. , Studio 360 (radio), 25/06/2010.
  2. Ntone Edjabe's biography on Cofeebeans Routs: "He is also a basketball coach, and was coach to another of our contributors Akin Omotoso during his studies at the University of Cape Town."
  3. Ntone Edjabe's biography Archived 24 Septemba 2006 at the Wayback Machine. as facilitator of Time of the Writer 2004.
  4. The programme Abramowitz Artist-in-Residence at MIT
  5. "Africa's pioneering radio station". www.bushradio.co.za. Iliwekwa mnamo 2018-05-25. 
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ntone Edjabe kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.