Nenda kwa yaliyomo

Nostradamus

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Uchoraji wa Nostradamus.

Michel de Nostredame (anajulikana zaidi kama Nostradamus; 14 au 21 Desemba 1503 - 2 Julai 1566) alikuwa mfamasia na tabibu wa Ufaransa, pia mnajimu na mwaguzi au mtabiri wa mambo yajayo.

Alizaliwa huko Provence akafa kwa edema hukohuko Provence.

Anajulikana kwa kitabu chake Les Prophéties (matabiri) ambayo ni mkusanyiko wa beti 942 zinazodaiwa kutabiri mambo yajayo. Kitabu hicho kilitolewa mara ya kwanza mwaka 1555. Tangu mwaka ule kitabu hicho kilichapishwa mara kwa mara. Kwa miaka mingi, kuna watu walioamini kwamba Nostradamus alitabiri matukio mbalimbali katika historia. Mara nyingi walifikia hitimisho hili kwa kutumia mbinu za kupindisha maandiko yake kwa namna ya kupendekeza kwamba alitabiri siku zijazo.

Lakini mara nyingi watu waliamini kuona utabiri baada ya tukio kutokea; hakuna mfano kwamba mtu yeyote aliweza kutambua tukio kabla halijatokea. [1]

  1. Lemesurier, Peter, The Unknown Nostradamus, 2003

Tovuti za nje

[hariri | hariri chanzo]