Tambazi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Tambazi mguuni - baada ya kuminya ngozi alama inabaki kwa muda

Tambazi (ing. oedema, edema) ni maradhi inayosababisha uvimbe kwenye mwili. Inaonekana hasa mkononi, mguuni na tumboni lakini inaweza kutokea pia ndani ya mwili.[1]

Inapatikana wakati viowevu (majimaji) vinatoka kwenye mishipa midogo mwilini na kukusanyika katika tishu yaani kati ya seli za mwili.[2]

Tambazi ya mapafu (ing. pulmonary edema ) ni mkusanyiko wa majimaji kwenye mapafu[3]. Hali hii ni hatari kwa sababu kiowevu ndani ya mapafu inaleta matata ya kupumua, inapunguza oksijeni inayopatikana mwilini na kama ni nyingi sana inaweza kumwua mtu[4].

Tambazi tumboni huitwa ascites.[5]

Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tambazi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  1. Dugdale, David (2013-04-21). "Foot, leg, and ankle swelling". Medline Plus. National Institutes of Health. Iliwekwa mnamo 2015-01-03. 
  2. "Edema". Mayo Clinic. 2014-09-19. Iliwekwa mnamo 2015-01-03. 
  3. Chen, Michael (2014-05-13). "Pulmonary edema". Medline Plus. National Institutes of Health. Iliwekwa mnamo 2015-01-03. 
  4. Ware LB, Matthay MA (December 2005). "Clinical practice. Acute pulmonary edema". N. Engl. J. Med. 353 (26): 2788–96. PMID 16382065. doi:10.1056/NEJMcp052699.  Check date values in: |date= (help)
  5. Longstreth, George (2013-10-13). "Ascites". Medline Plus. National Institutes of Health. Iliwekwa mnamo 2015-01-03.