Nightshift

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
“Nightshift”
“Nightshift” cover
Single ya Commodores
kutoka katika albamu ya Nightshift
B-side "I Keep Running"
Imetolewa Januari 31, 1985
Aina Soul, funk
Urefu 5:04 (toleo la albamu)

4:19 (7" haririo la single)

Studio Motown
Mtunzi Walter Orange
Dennis Lambert
Franne Golde
Mtayarishaji Dennis Lambert
Mwenendo wa single za Commodores
"Only You"
(1983)
"Nightshift"
(1985)
"Animal Instinct"
(1985)

"Nightshift" ni wimbo maarufu wa mwaka wa 1985 ambao uliimbwa na kundi zima la kina Commodores na vilevile jina la kibao ndiyo jina la albamu Nightshift. Wimbo ulitungwa kwa ajili ya manguli wa muziki Jackie Wilson na Marvin Gaye, wanamuziki maarufu wawili wa R&B ambao walifariki mwaka wa 1984.

Wimbo huu ndiyo wa kwanza kutamba kutoka kwa Commodores tangu safari ya kuondoka kwake Lionel Richie kutoka katika kundi hili. Pia ndiyo kibao kikubwa tangu kuondoka kwa Richie, imeshika nafasi ya tatu kwenye chati za Billboard Hot 100 na UK Singles Chart,[1] na kuibuka nafasi ya kwanza kwenye chati za Hot Black Singles.[2] Ijapokuwa bendi ilikuwa kinyume na studio yao katika kufanya maamuzi ya kutoa wimbo huu kama single,[3] Ilishinda katika Grammy Award mnamo 1985 kwa ajili ya "Best Vocal R&B Performance by a Duo/Group".

Kina Commodores waliurekodi upya wimbo huu mwaka wa 2010, lakini safari hii uliimbwa kwa ajili ya hayati Michael Jackson.[4]

Nafasi za chati

Chait (1985) Nafasi
iliyoshika
U.S. Billboard Hot 100 3
U.S. Billboard Hot Black Singles 1
Dutch Top 40 1[5]
UK Top 75 3

Matoleo mengine

Toleo la reggae la wimbo huu lilirekodiwa na Winston Groovy, huku mashairi yake yakibadilishwa na kuwa kama sehemu ya kumuenzi nguli wa muziki wa raggae hayati Bob Marley.[6]

Mshindi wa Tuzo za Grammy na American Idol Fantasia alichukua sampuli ya wimbo huu na kuimbwa kwa ajili ya single yake mpya ya Lose to Win.

Marejeo

Viungo vya Nje


Kigezo:Commodores


Kigezo:1980s-pop-song-stub