Nenda kwa yaliyomo

Nguchiro Miraba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nguchiro miraba
Nguchiro miraba
Nguchiro miraba
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mammalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Carnivora (Wanyama mbua)
Nusuoda: Feliformia (Wanyama kama paka)
Familia: Herpestidae (Wanyama walio na mnasaba na Nguchiro)
Jenasi: Mungos
Spishi: M. mungo
(Gmelin, 1788)
Msambazo wa nguchiro miraba
Msambazo wa nguchiro miraba

Nguchiro miraba (Mungos mungo)) ni mnyama mlanyama mdogo anayeishi hasa katika nchi za Afrika kusini kwa Sahara. Hula wadudu na wanyama wengine wadogo. Tofauti na nguchiro wengine wanaoishi mara nyingi maisha ya pekee, nguchiro miraba huishi kwa makundi ya wanyama 10 hadi 20.

Uainishaji

[hariri | hariri chanzo]

Wanaingia ufalme Animalia, Jamii ya Chordata, Kundi la mammalia, Mpango wa carnivora, familia ya Herpestidae, Jenasi ya Mungos, na Spishi ya Mungos mungo.

Nguchiro miraba au (Mungos mungo) wanaishi Afrika Mashariki na Kati lakini tu mahali ambapo kuna mvua. Nguchiro miraba wanaishi katika maeneo ya majani, savanna, na misitu.

Nguchiro miraba anatumia mapango ya mchwa kuishi ndani, lakini wanatumia mapango ambayo wanachimba au wanapata. Wanaweza kuishi katika mapango ambayo walichimba pia. Pango moja linaweza kuwa na nguchiro miraba kumi au ishirini ndani na pango moja linaweza kuwa na milango tisa na vyumba vingi.

Kiunzi cha mifupa cha Nguchiro

Nguchiro miraba wanakula mende, jongoo, na wadudu wengine. Wanakula mayai, baadhi ya matunda, na panya pia. Lini nguchiro miraba wanaona mnyama kama konokono wanagonga ni na mwamba ili kuivunja na kula nyama ya ndani. Lini nguchiro miraba wanaona wadudu masmuma wata kutika kwenye uchafu kwa hivyo wanaweza kula ni na sio kufa.

Nguchiro miraba wanaishi katika familia na sio wenyewe. Katika familia moja za nguchiro miraba kuna wanyama kumi au ishirini. Nguchiro miraba ni kahawia na nyeusi mgongo wao. Wao wana uzito kuanzia moja kilo mpaka tatu kilo. Nguchiro miraba wana urefu wa kuanzia sentimita thelathini mpaka sentimita araobaini na tano. Wanaweza kuishi miaka kumi na mbili. Wanaweza kukimbia kilomita thelathini kwa saa. Nguchiro miraba wanabeba ujauzito kwa mezi wiwili na wanaweza kuwa na watoto kati ya wawili na sita. Watato wanaishi mbali na wazazi wao wakati wanapofikisha miezi mitatu. Nguchiro miraba hawako katika hatari ya kupotea kwa sababu wao ni wagumu na wanakula wadudu.  

Mwenendo

[hariri | hariri chanzo]

Nguchiro miraba na ngiri hufanya kazi pamoja. Hii ni nzuri kwa nguchiro miraba kwa sababu wanapata chakula na ngiri wanapata kusafishwa. Ngiri hulala pembeni mwa familia ya nguchiro miraba na wanakula vimelea vyote katika mwili wa ngiri. Pia ngiri wanalinda familia ya nguchiro miraba kwa hivyo ngiri wengi wanaweza kusafishwa pia. Nguchiro miraba wanaweza kusema na kila mtu wa familia yao. Kwa sababu nguchiro miraba wanaishi katika familia kubwa ni muhimu waweze kuwasiliana na kila mmoja ili wanaweze kuishi salama.

Mwindaji wa Nguchiro Miraba

[hariri | hariri chanzo]

Mbwa mwitu, mbweha, fisi, mamba, chui, simba, mbweha na tai wote wanakula nguchiro miraba.

Nguchiro Miraba na Nyoka

[hariri | hariri chanzo]

Nyoka wanaweza kula nguchiro miraba pia kwa hiyo nguchiro miraba ni wepesi na wanaweza kukwepa kugongwa na nyoka. Baada ya muda nyoka huchoka, na nguchiro miraba wanamuua nyoka. Pia aina nyingine za mongofu hawawezi kudhuriwa na sumu ya nyoka. Nguchiro Miraba pia wana ngozi yao inawalinda kwa kuumwa na nyoka.

Matumizi ya Binadamu ya Nguchiro Miraba

[hariri | hariri chanzo]

Katika Afrika nguchiro miraba wanaweza kutumiwa na wanadamu kuua mende, jongoo, na wadudu wengine. Lakini hawawezi kutumia kama wanyama wa kufugwa. Katika mwaka elfu moja na mia nane na themanini tatu nguchiro miraba walitumiwa na watu kuua mende, jongoo, na wadudu katika Hawaii lakini waliua wanyama wote wadogo. Kwa hivyo sasa huwezi kuwa na zaidi mongofu katika nchi ya Marekani na Australia.

Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nguchiro Miraba kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.