Ng'ambo
Mandhari
Ng'ambo inamaanisha mahali palipo upande mwingine wa kizuizi fulani kama mto, bonde, mlima au bahari. Mara nyingi inatumiwa kutaja sehemu iliyo mbali sana, kwa mfano "alikwenda kusoma ng'ambo" yaani katika nchi nyingine, kwa kawaida hata nje ya Afrika.
Neno latumiwa pia kama jina la maeneo kama kata, vijiji au vitongoji katika sehemu mbalimbali za Afrika ya Mashariki.
- kata ya Ng'ambo (Tabora mjini)
- kata ya Ng'ambo (Moshi Mjini)
- kata ya Ng'ambo (Baringo)