Netflix
Netflix ni kampuni ya Marekani inayotoa huduma ya kutazama filamu na vipindi vya runinga kupitia intaneti.
Wateja wananunua huduma kwa muda wa miezi fulani halafu wanaweza kutazama filamu zilizomo katika hazinadata ya Netflix.
Mteja hawezi kupakua media hizo yaani hawezi kubaki na nakala ya filamu bali anaiangalia moja kwa moja.
Kwenye mwaka 2021 Netflix ilikuwa na wateja milioni 209 kote duniani[1][2].
Marejeo[hariri | hariri chanzo]
- ↑ Kastrenakes, Jacob. "Netflix subscriber growth is stalling as it runs low on hits", The Verge, April 20, 2021.
- ↑ Katz, Brandon. "Netflix Growth Is Slowing, But Its Customers Remain the Most Loyal of All", Observer, April 30, 2021.