Nenda kwa yaliyomo

Naziha al-Dulaimi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Naziha Jawdet Ashgah al-Dulaimi ( 1923 - 9 Oktoba 2007) alikuwa mwanzilishi wa mwanzo wa vuguvugu la kutetea haki za wanawake wa Iraq . Alikuwa mwanzilishi mwenza na raisi wa kwanza wa Iraqi Women League, [1] waziri mwanamke wa kwanza kwenye historia ya kisasa ya Iraq, na waziri wa kwanza wa baraza la mawaziri mwanamke kwenye ulimwengu wa Kiarabu. [2]

Al-Dulaimi, ambaye babu yake aliondoka al-Mahmudia (kati ya Baghdad na Babeli), alizaliwa huko Baghdad, ambapo familia yake ilikuwa na makazi mwishoni mwa karne ya 19. Alisomea udaktari katika Chuo cha Kifalme cha tiba (baadaye kiliunganishwa na Chuo Kikuu cha Baghdad ). [3] Alikuwa mmoja wa wanafunzi wachache wa kike katika Chuo cha Matibabu. Wakati huo alijiunga na "Jumuiya ya Wanawake ya Kupambana na Ufashisti na Unazi" na alihusika kikamilifu kwenye kazi iyo. Baadaye, wakati jumuiya ilibadilisha jina lake kuwa "Chama cha Wanawake wa Iraqi," akawa mwanachama wa kamati yake ya utendaji.

Marejeleo

[hariri | hariri chanzo]
  1. Al-Ali, Nadje (2012-07-01), Arenfeldt, Pernille; Golley, Nawar Al-Hassan (whr.), "The Iraqi Women's Movement: Past and Contemporary Perspectives", Mapping Arab Women's Movements, American University in Cairo Press, uk. 107, doi:10.5743/cairo/9789774164989.003.0005, ISBN 978-977-416-498-9, iliwekwa mnamo 2020-03-08
  2. "Dr. Naziha Jawdet Ashgah al-Dulaimi | Women as Partners in Progress Resource Hub". pioneersandleaders.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-03-17. Iliwekwa mnamo 2020-03-08.
  3. "Dr. Naziha Jawdet Ashgah al-Dulaimi | Women as Partners in Progress Resource Hub". pioneersandleaders.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-03-17. Iliwekwa mnamo 2020-03-08."Dr. Naziha Jawdet Ashgah al-Dulaimi | Women as Partners in Progress Resource Hub" Archived 17 Machi 2020 at the Wayback Machine..
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Naziha al-Dulaimi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.