Nassau (Bahamas)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nassau

Boma la Charlotte juu ya mji Nassau (Bahamas)
Habari za kimsingi
Mkoa Eneo la mji mkuu Managua (Departmento Managua)
Anwani ya kijiografia Latitudo: 12°8′12″N - Longitudo: 86°15′5″W
Kimo 55 - 900 m juu ya UB
Eneo - Manisipaa 544 km²
- mji 173.7 km²
Wakazi 1,380,100 (2001)
Msongamano wa watu watu 2,537 kwa km²
Simu +505 (nchi), 2 (mji)
Mahali

Nassau ni mji mkuu wa Bahamas ambayo ni nchi ya visiwani katika Atlantiki mbele ya mwambao wa Kuba na Florida. Nassau ina wakazi 210,832 ni pia mji mkubwa wa nchi hii ndogo. Iko kwenye kisiwa cha New Providence.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Nassau iliundwa na walowezi Waingereza mwaka 1656 ikaitwa "Charlestown" kwa heshima ya mfalme Charles II wa Uingereza. Jina likabadilishwa 1695 kuwa Nassau kwa heshima ya mfalme William III wa Uingereza kutoka familia ya Orange-Nassau.

Wakati wa karne ya 18 Nassau ilikuwa kimbilio cha maharamia wa Karibi. Kilele chake kilikuwa kipindi kifupi cha "jamhuri ya maharamia" chini ya mashuhuri Blackbeard (ndevu nyeusi). Serikali ya Uingereza ulipaswa kungilia kati na kuwafukuza mwaka 1718. Mji ulishambuliwa mara nyingi na Wahispania na kuchomwa. Mwisho wa karne ya 18 wakimbizi Waingereza kutoka bara ya Amerika Kaskazini wasiokubali uasi wa MArekani walihamia Bahamas hivyo Nassau ikakua.

Mwisho wa utumwa ulikuwa pigo kwa uchumi wa wenye mashamba visiwani na mji wa Nassau ukawa maskini.

Kwa muda mrefu sehemu ya mapato ya Nassau ilikuwa biashara ya upenyezi yaani kuingiza bidhaa Marekani bila kulipa ushuru. Biashara hii ilistawi mno wakati ambako pombe ilipiogwa marufuku Marekani kati ya 1919 na 1933.

Tangu miaka ya 1950 uchumi wa Nassau ulibadilika ikawa utalii hasa ya watalii kutoka Marekani. Tangu mwisho wa karne Nassau imekuwa kitovu cha benki za kimataifa.

Makala hii kuhusu maeneo ya Bahari ya Karibi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Nassau (Bahamas) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.