Nancy Lynch

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Nancy Ann Lynch (amezaliwa Januari 19, 1948) [1] ni mwanahisabati, mwananadharia, na profesa katika Taasisi ya Teknolojia ya Massachusetts . Yeye ni Profesa wa NEC na mkuu wa idara ya sayansi ya uhandisi EECS katika Maabara ya Sayansi ya Kompyuta na MIT.

Elimu na maisha ya awali[hariri | hariri chanzo]

Lynch alizaliwa Brooklyn, na alikua na taaluma ya Hisabati. Aliudhuria chuo cha Brooklyn College and MIT, ambapo alihitimu na shahada ya uzamili mwaka 1972 chini ya Albert R. Meyer.

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Alihudumu katika kitivo cha hesabu na sayansi ya kompyuta katika vyuo vikuu vingine kadhaa, ikijumuisha Chuo Kikuu cha Tufts, Chuo Kikuu cha Kusini mwa California, Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Florida, na Taasisi ya Teknolojia ya Georgia (Georgia Tech), kabla ya kujiunga na kitivo cha MIT mnamo 1982. Tangu wakati huo, amekuwa akifanya kazi kwa kutumia taaluma yake ya hisabati kutengeneza mifumo mbalimbali.

Bibliografia[hariri | hariri chanzo]

Lynch, Nancy; Merritt, Michael; Weihl, William; Fekete, Alan (1994). Atomic Transactions. San Mateo, California: Morgan Kaufmann. ku. 476. ISBN 9781558601048. 

Lynch, Nancy A. (1998). Distributed Algorithms (toleo la 2nd). San Francisco, California: Kaufmann. ISBN 978-1558603486.  Unknown parameter |url-access= ignored (help)

Kaynar, Dilsun; Lynch, Nancy; Segala, Roberto; Vaandrager, Frits (2011). The Theory of Timed I/O Automata (toleo la 2nd). San Rafael, California: Morgan & Claypool. uk. 137. ISBN 9781608450039. 

Marejeleo[hariri | hariri chanzo]

  1. Who's who of American women. Marquis Who's Who, 1973. p. 587.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nancy Lynch kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]