Namba isiyowiana

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Kipeuo mraba cha 2 ni namba isiyowiana

Namba isiyowiana (en:irrational number[1]) ni namba halisi ambayo haiwezi kuonyeshwa kama wianisho safi baina namba kamili.

Mifano mashuhuri ni kipeuo mraba cha 2 na namba ya duara π (Pi). Kwa mfano Pi ikiandikwa kwa namna ya desimali inaanza hivi 3.14159265358979 .... lakini kamwe haiwezi kuonyeshwa kikamilifu kwa kuongeza tarakimu baada ya nukta.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Jina la Kilatini-Kiingereza "irrational" haimaanishi "bila akili" ("ratio" kama akili, hekima, en:reason) lakini "bila wianisho" ("ratio" kama uwiano, relation)

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu: