Mwingi wa Habari

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mwingi wa Habari
Mwingi wa Habari Cover
Studio album
Imetolewa Octoba 18, 2013
Imerekodiwa 2012/2013
Aina Hip hop, Hip hip ya kujitambua
Lebo Tattoo Records, Bongo Records
Mtayarishaji Palla, P. Funk, Soul Plugger, Bunduki Midundo

Mwingi wa Habari ni jina la kutaja albamu ya kwanza ya msanii wa muziki wa hip hop kutoka nchini Tanzania - P. the MC. Albamu ilitolewa kupitia studio za Tattoo Records na Bongo Records. Albamu ilianza kufanyiwa harakati za uuzaji mnamo tar. 18 Oktoba, 2013.

Katika albamu hii amepata kushirikisha wasanii wengine wa hip hop na Bongo Flava kutoka Tanzania, ikiwa ni pamoja na Cianah, Mansu L, Nikki Mbishi, Songa, One the Incredible, 10 Kiraka, na Maulo na wengine wengi. Katika albamu hii, kuna nyimbo zimefanywa kuchukuliwa sampuli kutoka katika nyimbo za manguli wa muziki kutoka nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na sauti kutoka kwa hayati Marijani Rajabu na Remmy Ongala. Hakika ni mapinduzi makubwa katika hali ya kufanya sampuli ya nyimbo zingine.


Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]