Nenda kwa yaliyomo

Mwezi wa Ufahamu wa Saratani ya Matiti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Saratani hiyo ilivyo.

Mwezi wa Ufahamu wa Saratani ya Matiti ulianzishwa katika juhudi za kuongeza uelewa wa kimataifa kuhusu saratani ya matiti.

Oktoba imeteuliwa ikizingatiwa kama Oktoba ya rangi ya waridi kwa muda. Katika mwezi huu, jitihada zinafanywa kuwaelimisha watu duniani kote kuhusu ugonjwa huo na jinsi ya kujua dalili na mabadiliko ya mapema yanayohusiana na saratani ya matiti. Pia unajulikana kama Mwezi wa Uhamasishaji wa Saratani ya Matiti, hii ni kampeni ya kimataifa ya afya inayoandaliwa kila mwaka na mashirika ya misaada ya saratani ya matiti ili kuongeza ufahamu wa ugonjwa huo na kutafuta pesa kwa ajili ya utafiti wa vianzishi vyake, kinga, vipimo na matibabu. [1]

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Tukio hilo lilianza kama Mwezi wa Kitaifa wa uhamasishaji wa Saratani ya Matiti mwaka wa 1985 Oktoba. Iliwakilisha ushirikiano kati ya Jumuiya ya Saratani ya marekani na idara ya dawa ya Imperial Chemical Industries, kukuza mammogram kama zana bora zaidi katika vita dhidi ya saratani ya matiti. Aliyekuwa Mama wa Kwanza wa Marekani Betty Ford, aliyenusurika na saratani ya matiti, alisaidia kutilia mkazo zaidi mpango huo. Miaka saba baadaye, utepe wa rangi ya waridi ulitumiwa mara ya kwanza  kama ishara ya kampeni. [2]

Utepe wa waridi

[hariri | hariri chanzo]

Asili ya utepe wa waridi ni wa zamani hata kabla ya uvumbuzi wa mwezi wa uhamasisho wa saratani ya matiti. Chanzo cha awali cha ishara hii ulitokea mwaka wa 1979 wakati mke wa mateka wa Irani alipofunga utepe za manjano kwenye miti iliyokuwa kwenye uwanja wake kama ishara ya matumaini yake ya kurudi salama kwa mumewe nyumbani.

Baadaye, wanaharakati wa virusi vya ukimwi walivaa utepe za manjano kama ishara ya uungano wakati wa vita vya Ghuba, lakini baadaye walizibadilisha na kutumia rangi nyekundu iliyoiva. Utepe pia ulitumiwa katika Tuzo za Tony kama ishara ya msaada kwa wale wanaougua virusi vya ukimwi. Kitengo cha New York Times kikatambua 1992 kama "Mwaka wa utepe".

Ingawa leo rangi ya waridi ni sawa na ufahamu wa saratani ya matiti, rangi ya awali ya utepe ilikuwa peach. Mwanzoni mwa mwaka wa 1992, wakati huo mhariri mkuu wa gazeti la Self, Alexandra Penney, alikuwa akifanyia kazi toleo la pili la kila mwaka la jarida hilo lililotolewa kwa mwezi wa kuhamasisha saratani ya matiti. Evelyn Lauder, aliyekuwa makamu wa rais wa shirika huko Estée Lauder na yeye mwenyewe aliyenusurika na saratani ya matiti, aliunga mkono wazo la kusambaza utepe nchini nzima.

Hata hivyo, Charlotte Haley alikuwa wa kwanza kuja na wazo la kuunda utepe. Alitengeneza utepe za rangi ya peach zilizotengenezwa kwa mikono kwa heshima ya mama yake, dada yake, na nyanyake, ambao walikuwa wamekabiliana na saratani ya matiti. Alisambaza seti za utepe pamoja na kadi za habari kuhusu bajeti ya taasisi ya Kitaifa ya Saratani na umuhimu wa kinga. Penney alijua kuhusu kazi yake na akatoa msaada wa kitaifa, lakini Haley alikataa, akiamini kuwa ushirikiano ungekaa kama wa kibiashara sana. [3]

Baadaye, rangi ya waridi ilihusishwa na mpango uliozinduliwa na jarida la Self na Estée Lauder. Tangu wakati huo, utepe na rangi ya waridi zimekuwa alama zinazotambulika sana za ufahamu wa saratani ya matiti. Licha ya hayo moja ya mashirika ya kimataifa ya saratani ya matiti inayoongoza ulimwenguni yamekuwa yakitumia rangi ya waridi tangu kuvumbuliwa kwake mnamo 1982. [4]

Saratani ya matiti ni aina ya pili ya saratani ulimwenguni inayowapata zaidi wanawake. Mwaka 2022, kulikuwa na kesi mpya 2,296,840 za saratani ya matiti kati ya wanawake, na idadi kubwa zaidi kwenye nchi kama vile Uchina, Marekani na India. Ufaransa ilikuwa na kiwango kikubwa zaidi cha saratani ya matiti mwaka huo. [5]

Mashirika yanayounga mkono Mwezi wa Kupinga Saratani ya Matiti

[hariri | hariri chanzo]
Mashirika ya Kimataifa
[hariri | hariri chanzo]
  • American Cancer Society (ACS) - Shirika hili hutoa rasilimali za elimu na msaada kwa wale wanaougua saratani ya matiti na huandaa matukio wakati wa Oktoba ya Rangi ya Pinki.
  • Susan G. Komen Foundation - Imedhamiria katika utafiti, elimu, na msaada kwa wale wanaougua saratani ya matiti.
Mashirika ya Kitaalamu
[hariri | hariri chanzo]
  • Breast Cancer Now (Uingereza) - Shirika hili hutoa taarifa, msaada, na fedha za utafiti.
  • Australian Breast Cancer Network (Australia) - Hutoa rasilimali na msaada kwa walio na saratani ya matiti nchini Australia.
  • Žena uz ženu (Serbia) - Kupitia kampeni, matukio ya umma, na ushirikiano na taasisi za afya, shirika hili linajitahidi kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa kugundua saratani ya matiti mapema, pamoja na kutoa msaada wa vitendo na kihisia kwa wanawake wanaougua.
Watu Maarufu na Mabalozi
[hariri | hariri chanzo]
  • Beti Ford - Mke wa Rais wa zamani wa Marekani, ambaye aliepuka saratani ya matiti, alicheza jukumu kuu katika kukuza uelewa kuhusu ugonjwa huu.
  • Angelina Jolie - Muigizaji na mtetezi ambaye amezungumzia wazi kuhusu uzuiaji wa saratani ya matiti.
Makampuni na Brands
[hariri | hariri chanzo]
  • Estée Lauder - Maarufu kwa kampeni zake za kimataifa kuhusu saratani ya matiti, ikijumuisha mauzo ya bidhaa kwa ajili ya kukusanya fedha.
  • Nike - Kampuni hii mara nyingi inasaidia kampeni za mwezi kwa kupandisha uelewa kupitia bidhaa maalum na michango.
  • Meridianbet - Kupitia ushirikiano wao, wanasaidia kuongeza uelewa kuhusu saratani ya matiti na kutoa msaada kwa wale wanaougua.[6]
  • Lindex Serbia - Kampuni hii mara nyingi inashiriki katika kampeni za kukusanya fedha na hutoa sehemu ya mapato ya mauzo ya bidhaa maalum kwa ajili ya kusaidia utafiti na kinga ya saratani ya matiti.
Wataalamu wa Afya na Taasisi
[hariri | hariri chanzo]
  • Pharmaceutical Chamber of Serbia - Huandaa na kushiriki katika matukio na shughuli mbalimbali zinazolenga kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa kinga na kugundua saratani ya matiti mapema.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. "Breast Cancer Awareness Month | UICC". www.uicc.org (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-07-12.
  2. "A Glimpse of Breast Cancer Awareness Month's History". Brevard Health Alliance (kwa American English). 2019-10-17. Iliwekwa mnamo 2024-07-12.
  3. "History of the Pink Ribbon". Breast Cancer Action (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-07-12.
  4. https://www.komen.org/uploadedFiles/Content_Binaries/The_Pink_Ribbon_Story.pdf. {{cite web}}: Missing or empty |title= (help)
  5. "Breast cancer statistics | World Cancer Research Fund International". WCRF International (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-07-12.
  6. "October, the month of solidarity and awareness on breast cancer". www.mfa.com.mt (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-08-28.
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mwezi wa Ufahamu wa Saratani ya Matiti kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.