Nenda kwa yaliyomo

Mweta

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mweta ni jina la Kitanzania. Asili yake ni kabila la Wapare. Mweta maana yake ni kijito kinachotiririsha maji. Jina hili limeenea hadi kwa makabila ya Wasambaa na Wanguu.

Jina lingine linalofanana na hilo ni Shemweta ambalo hutumiwa zaidi na Wasambaa, hasa waishio maeneo ya Bumbuli katika wilaya ya Bumbuli.