Mwenge wa Uhuru

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
mwenge wa uhuru katika stempu ya barua ya shilingi 20

Mwenge wa uhuru[1] (kwa Kiingereza Uhuru Torch) ni mojawapo ya alama za kitaifa za Tanzania [2].

Ina muundo wa tochi ya mafuta ya taa ambayo inaashiria uhuru na mwanga. Mwenge wa uhuru ulinyanyuliwa katika kilele cha Mlima Kilimanjaro mnamo Desemba 9, 1961 na shujaa Brigedia Alexander Nyirenda ikiashiria kuangaza nchi na kuvuka mipaka kuleta matumaini palipo kukata tamaa, upendo palipo uadui na heshima palipo chuki. Sababu ya huyu brigedia kunyanyua mwenge huu ni kuonesha fahari ya nchi na pia kuleta matumaini kwa Watanzania wote kwa kutokata tamaa, kupendana, kuheshimiana na kutogombana ikimaanisha kuwa na ushirikiano.

Mbio za Mwenge wa Uhuru hufanyika kila mwaka kuanzia maeneo mbalimbali nchini.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Mwenge wa uhuru
  2. [https://www.bing.com/search?q=coat+of+arm+in+swahili&qs=n&form=QBRE&sp=-1&ghc=1&lq=0&pq=coat+of+arm+in+swahili&sc=10-22&sk=&cvid=C0CC9CAD9BCD4870ADA318A829D18AE6&ghsh=0&ghacc=0&ghpl=