Nenda kwa yaliyomo

Muna Lee (mwanamichezo)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Muna Lee(mwanamichezo))

Makala hii inahusu mwanariadha wa Marekani. Kwa makala ya mwandishi wa Puerto Rico, angalia Muna Lee (mwandishi).

Rekodi za medali

Muna Lee (aliye nyuma) akishindana na Allyson Felix katika majaribio ya Olimpiki
Anawakilisha nchi MarekaniMarekani
Riadha ya Wanawake
Mashindano ya Mabingwa wa Dunia ya IAAF
Dhahabu 2005 Helsinki 4x100 m

Muna Lee (alizaliwa Little Rock, Arkansas, 30 Oktoba 1981) ni mwanariadha wa mbio fupi fupi wa Marekani.

Lee alishinda medali ya dhahabu kama mwanachama wa timu ya Wanawake ya mbio 4 x 100m katika mbio ya Mashindano ya Mabingwa wa Dunia katika Riadha katika mwaka wa 2005. Alikimbia vizuri sana katika mbio za majaribio ya Olimpiki ya 2004,akikimbia kwa kasi katika mkondo wa mwisho na kupita wanariadha wenzake na kushinda nafasi katika timu ya Olimpiki. Aliendelea na akawa nambari 7 katika Michezo ya Olimpiki.

Mwanariadha wa Marekani: Muna Lee

Alishiriki katika michezo ya Olimpiki ya 2008,Beijing akikimbia mbio ya 100m. Katika mbio ya mchujo ya awamu ya kwanza,alikuwa nambari ya kwanza akiwa mbele ya Anita Pisone na Guzel Khubbieva katika muda wa 11.44 s na kuweza kuhitimu awamu ya pili. Katika awamu ya pili ya mchujo aliboresha muda wake ukawa 11.08 na akamaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Sherone Simpson na kuhitimu kukimbia katika nusu fainali. Katika nusu fainali alikimbia na muda wa 11.06s nyuma ya Shelly-Ann Fraser akahitimu kukimbia katika fainali,alichukua nafasi ya tano katika fainali hiyo na muda wa sekunde 11.07 .

Yeye alichukua nafasi ya pili katika Mashindano ya Mabingwa wa Marekani (akiwa nyuma ya Carmelita Jeter) na akahitimu kukimbia katika Mashindano ya Mabingwa katika Riadha wa Dunia wa 2009. Wiki moja kabla ya Mashindano ya Mabingwa wa Dunia ,Lee alikuwa mmoja wa wanawake katika timu ya mbio ya 4 x 100 waliokimbia kwa muda ulio kasi sana katika miaka kumi na miwili. Lauryn Williams, Allyson Felix, Lee na Jeter walimaliza kwa muda wa sekunde 41.58, kuwapa nafasi ya nane kwenye orodha ya muda bora kabisa. [9]

Ubora wa binafsi

[hariri | hariri chanzo]
  • Mbio ya mita 100 - 10.85s (2008)
  • Mbio ya mita 200 - 22.01s (2008)
  1. ^ a b Athlete biography: Muna Lee, beijing2008.cn,
  2. ^ Morse, Parker (2009-06-27). Jeter and Rodgers take 100m titles in Eugene - US Champs, . IAAF.
  3. ^ Wenig, Jörg (2009-08-08). US quartet blasts 41.58 in the 4x100 as Wlodarczyk improves to 77.20m in Cottbus. Archived 10 Agosti 2009 at the Wayback Machine. IAAF.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]