Allyson Felix

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Allyson Michelle Felix OLY (alizaliwa Novemba 18, 1985)[1] ni mwanariadha wa Marekani. Kutoka mwaka 2003 hadi 2013, alibobea kwenye mbio za mita 200 na taratibu akahamia kwenye mbio za mita 400 kwenye maisha yake ya kazi. Kwa orodha yake ya mikimbio, mita 100, mita 4 *100 mbio fupi fupi na mita 4*400 mbio fupi fupi [2]. Kwenye mita 200, alikuwa ni bingwa wa 2012 wa olimpiki, na bingwa wa dunia mara tatu (2005-2009), mshindi mara mbili wa medali ya fedha (2004 na 2008) na mwaka 2011, medali ya shaba . Kwenye mita 400, alikuwa bingwa wa dunia mwaka 2015, 2011 mshindi wa medali ya fedha, 2016, mshindi wa medali ya fedha  kwenye olimpiki, 2017 mshindi wa medali ya shaba na 2020, mshindi wa medali ya shaba kwenye olimpiki.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. USA Track & Field - Allyson Felix (usatf.org)
  2. Allyson Felix (teamusa.org)