Mukulu
Mukulu ni kata ya Wilaya ya Iramba katika Mkoa wa Singida, Tanzania.
Kata ya Mukulu ina jumla ya vijiji vitatu, navyo ni Simbalungwala, Mukulu na Motomoto. Katika kata hiyo kuna jumla ya vitongoji 11: vinne katika kijiji cha Simbalungwala navyo ni Kilambazi, Magugu, Shuleni na Ulongo. Kijiji cha Mukulu kina vitongoji vinne pia, navyo ni Mukulu A, Mkulu B, Mukulu C na Mukulu D (Kagera). Kijiji cha Motomoto kina jumla ya vitongoji vitatu navyo ni Stefano, Mtandao na Mwampiti.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 7,392 [1].
Shughuli za kiuchumi ni kilimo na ufugaji. Katika kata ya Mukulu kuna uzalishaji mkubwa wa mahindi, alizeti na dengu. Kuna ufugaji wa ng'ombe, mbuzi, kondoo na kuku.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]![]() |
Kata za Wilaya ya Iramba - Mkoa wa Singida - Tanzania | ![]() |
---|---|---|
Kaselya | Kidaru | Kinampanda | Kiomboi | Kisiriri | Kyengege | Maluga | Mbelekese | Mgongo | Mtekente | Mtoa | Mukulu | Ndago | Ndulungu | Ntwike | Old-Kiomboi | Shelui | Tulya | Ulemo | Urughu |
![]() |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Singida bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mukulu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno. |