Nenda kwa yaliyomo

Mtumiaji:Lucas559/Lupus

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Lucas559/Lupus
Mwainisho na taarifa za nje
Matamshi
Kundi MaalumuRheumatolojia
DaliliMaumivu na kuvimba kwa viungo, homa, maumivu ya kifua, kukatika kwa nywele, vidonda vya mdomoni, kuvimba kwa tezi za limfu, kuhisi uchovu, upele mwekundu[1]
Miaka ya kawaida inapoanzaUmri wa miaka 15-45[1][2]
MudaUgonjwa unaotokea kwa kipindi cha muda mrefu[1]
VisababishiHavijulikani vyema[1]
Njia ya kuitambua hali hiiKulingana na dalili na vipimo vya damu[1]
Dawadawa zisizo za steroidi (NSAIDs), kortikosteroidi (corticosteroids), dawa za kuzuia mfumo wa kinga (immunosuppressants), hidroksiklorokwini (hydroxychloroquine), methotrexate[1]
Utabiri wa kutokea kwakeKuishi kwa miaka 15 ~ asilimia 80%[3]
Idadi ya utokeaji wakewatu 2–7 kwa kila 10,000[2]

Ugonjwa wa Mapaku Mekundu (Lupus), uaojulikana kwa lugha ya kitaalamu kama systemic lupus erythematosus (SLE), ni ugonjwa wa kinga ya mwili kushambulia seli za mwili kimakosa, ambapo mfumo wa kingamwili hushambulia kimakosa tishu zenye afya katika sehemu nyingi za mwili.[1] Dalili zake hutofautiana kati ya watu na zinaweza kuwa ndogo hadi kali sana.[1] Dalili zake za kawaida zinajumuisha maumivu na kuvimba kwa viungo, homa, maumivu ya kifua, kukatika kwa nywele, vidonda vya mdomo, kuvimba kwa tezi za limfu, kuhisi uchovu na upele mwekundu ambao mara nyingi hupatikana kwenye uso.[1] Mara nyingi kuna vipindi vya kuwa na afya mbaya, vinavyoitwa kama vipindi vya hali ya afya kuwa mbaya zaidi (flares) na vipindi vya kutokuwepo kwa dalili zake (remission) ambapo kuna dalili chache tu.[1]

Visababishi vyake havifahamiki vyema. [1] Inafikiriwa kuwa vinahusisha jeni pamoja na mambo ya kimazingira.[4] Miongoni mwa watoto mapacha wanaofanana, ikiwa mmoja wao ameathiriwa, kuna uwezekano wa asilimia 24% kuwa huyo mwingine ataathiriwa pia.[1] Homoni za jinsia za kike, mwanga wa jua, uvutaji sigara, upungufu wa vitamini D na maambukizo fulani pia yanaaminika kuongeza hatari zake.[4] Mchakato huu unahusisha mwitikio wa kinga ambapo kingamwili hushambulia tishu za mtu mwenyewe.[1] Hizi kwa mara nyingi ni kingamwili za kupambana na kiini cha seli na husababisha uvimbaji.[1] Utambuzi wake unaweza kuwa mgumu na unategemea mchanganyiko wa dalili na vipimo vya maabara.[1] Kuna aina nyingine kadhaa za lupus erythematosus ikiwemo discoid lupus erythematosus, neonatal lupus, na subacute cutaneous lupus erythematosus..[1]

Ugonjwa huu hauna tiba[1] Matibabu yake yanaweza kujumuisha matumizi ya dawa zisizo za steroidi (NSAIDs), kortikosteroidi (corticosteroids),dawa za kuzuia mfumo wa kinga (immunosuppressants), hidroksiklorokwini (hydroxychloroquine), na (methotrexate.[1] Ingawa kortikosteroidi hufanya kazi vizuri kwa haraka, matumizi yake kwa muda mrefu husababisha madhara.[5] Dawa mbadala haijaonyeshwa kuathiri ugonjwa huu.[1] Umri wa kuishi ni mdogo kati ya watu wenye SLE.[6] SLE huongeza kwa kwa kiasi kikubwa hatari ya kupata ugonjwa wa miships ya moyo na hii ikiwa sababu ya kawaida ya kutokea kwa kifo.[4] Kwa matibabu ya kisasa, karibu asilimia 80% ya walioathiriwa wanaishi zaidi ya miaka 15.[3] Wanawake walio na lupus wana mimba ambazo ni hatari zaidi lakini wanawake hujifungua nyingi ya mimba hizo.[1]

Kiwango cha SLE hutofautiana kati ya nchi kutoka watu 20 hadi 70 kwa kila watu 100,000.[2] Wanawake wa umri wa kuzaa huathirika mara tisa zaidi kuliko wanaume.[4] Ingawa kwa kawaida huanza kati ya umri wa miaka 15 na 45, aina mbalimbali za umri zinaweza kuathirika.[1][2] Wale wenye asili ya Kiafrika, Karibea, na Uchina wako katika hatari zaidi kuliko wazungu.[4] [2] Viwango vya Ugonjwa katika nchi zinazoendelea havijulikani wazi.[7] Lupus ni neno la Kilatini linalomaanisha "mbwa mwitu": ugonjwa huu ulipewa jina hili katika karne ya 13, kwani upele huu ulifikiriwa kuwa na mwonekano kama ule wa kuumwa na mbwa mwitu.[8]

Marejeleo

[hariri | hariri chanzo]
  1. 1.00 1.01 1.02 1.03 1.04 1.05 1.06 1.07 1.08 1.09 1.10 1.11 1.12 1.13 1.14 1.15 1.16 1.17 1.18 1.19 1.20 "Handout on Health: Systemic Lupus Erythematosus". www.niams.nih.gov. Februari 2015. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 17 Juni 2016. Iliwekwa mnamo 12 Juni 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 Danchenko, N.; Satia, J.A.; Anthony, M.S. (2006). "Epidemiology of systemic lupus erythematosus: a comparison of worldwide disease burden". Lupus. 15 (5): 308–318. doi:10.1191/0961203306lu2305xx. PMID 16761508.
  3. 3.0 3.1 The Cleveland Clinic Intensive Review of Internal Medicine (tol. la 5). Lippincott Williams & Wilkins. 2012. uk. 969. ISBN 9781451153309. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 7 Januari 2020. Iliwekwa mnamo 13 Juni 2016.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. 4.0 4.1 4.2 4.3 4.4 Lisnevskaia, L; Murphy, G; Isenberg, D (22 Novemba 2014). "Systemic lupus erythematosus". Lancet. 384 (9957): 1878–88. CiteSeerX 10.1.1.1008.5428. doi:10.1016/s0140-6736(14)60128-8. PMID 24881804.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. Davis, Laurie S.; Reimold, Andreas M. (Aprili 2017). "Research and therapeutics—traditional and emerging therapies in systemic lupus erythematosus". Rheumatology. 56 (suppl_1): i100–i113. doi:10.1093/rheumatology/kew417. PMC 5850311. PMID 28375452.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. Murphy, G; Isenberg, D (Desemba 2013). "Effect of gender on clinical presentation in systemic lupus erythematosus". Rheumatology (Oxford, England). 52 (12): 2108–15. doi:10.1093/rheumatology/ket160. PMID 23641038.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. Tiffin, N; Adeyemo, A; Okpechi, I (7 Januari 2013). "A diverse array of genetic factors contribute to the pathogenesis of systemic lupus erythematosus". Orphanet Journal of Rare Diseases. 8: 2. doi:10.1186/1750-1172-8-2. PMC 3551738. PMID 23289717.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: unflagged free DOI (link)
  8. Chabner, Davi-Ellen (2013). The Language of Medicine. Elsevier Health Sciences. uk. 610. ISBN 978-1455728466. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-01-07. Iliwekwa mnamo 2020-08-04.