Mtumiaji:Jonny Frosty/Birutė Kalėdienė

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Birutė Kalėdienė akiwa kwenye mashindano ya Olimpiki Mwaka 1964

Birutė Kalėdienė ( Alizaliwa Novemba 2, 1934 Baltrušiai, Kaunti ya Marijampolė ) ni mrusha mkuki wa Kilithuania aliyestaafu na aliwahi kushinda medali ya fedha kwa Umoja wa Kisovieti katika Mashindano ya Uropa ya 1958. Alishiriki katika mashindano ya Olimpiki ya 1960 na 1964 na kumaliza katika nafasi ya tatu na ya nne.[1]

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Kalėdienė alizaliwa Lithuania mnamo mwaka 1934. Alianza mafunzo ya kurusha mkuki mnamo 1952 na alishinda mataji ya Soviet mnamo 1958-60. Mnamo 1958 alikua mwanariadha wa kwanza wa Kilithuania kuweka rekodi ya ulimwengu (57.49 m) na alichaguliwa kama mwanariadha wa Kilithuania wa mwaka huo.

Kalėdienė alistaafu mnamo 1966 na kuanza kufanya kazi kama mkufunzi huko Kaunas. Alikuwa mwanachama wa bodi ya klabu ya michezo ya Ąžuolyno Kaunas. Mnamo 2005, alishinda taji la ulimwengu katika kitengo cha F70 (Masters). [2]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Olympics Site Closed | Olympics at Sports-Reference.com". www.sports-reference.com. Iliwekwa mnamo 2022-12-10. 
  2. "Olympics Site Closed | Olympics at Sports-Reference.com". www.sports-reference.com. Iliwekwa mnamo 2022-12-10.