Mtumiaji:Jackson Augustine

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Jackson Kayanda (majina yote: Jackson Augustine Tryphone Kayanda), alizaliwa mnamo tarehe 17 Januari 1995 huko nchini Tanzania, mkoani Geita, katika mtaa wa Samina. Baba yake ni Augustine Tryphone Kayanda, na mama yake ni Resituta Mahilane Mhehemi.

Jackson aliishi na wazazi wake katika mtaa wa Samina hadi alipofikia umri wa miaka saba alipoanza shule rasmi katika shule ya msingi Mpomvu iliyo mtaa jirani katika kata ya Mtakuja.

Baada ya kifo cha baba yake mnamo mwaka 2002, alihamia Genge Saba kwa babu yake Tryphone Kayanda ambako aliendelea na elimu yake ya msingi darasa la pili mnamo 2003.

Mnamo 2008 alihitimu shule katika shule ya msingi Nyakamwaga, na kurejea Samina. Baadaye katika mwaka 2012 alipata fursa ya kujiunga na chuo cha ufundi cha Kirumba Technical Training College (KTTC), na alimaliza elimu ya ufundi stadi mnamo mwaka 2014 Desemba.

Katika Oktoba 2014 alianza kujiunga na dini na Machi 2015 alipokea ubatizo katika kanisa la SDA huko Pansias Mwanza. Baadaye katika Agosti hivi alirejea Samina tena.

Maisha yake ya 2016 hadi 2020 ni gumzo. Kwakweli yamekuwa ya aina ambayo haijawahi kutokea katika siku zote za nyuma, na hasa maisha yake ya miaka hii miwili; 2019 na 2020. Kwa hasa, tangu Julai 2019 alipoanza kupata matatizo ya kubaguliwa na kudhurumiwa na jamii yake ya Samina Geita na mitaa ya karibu. Yote hii kwa jumla ilionekana kutokana na ukosefu wa uhuru, hasa upande wa dini; kitu kilichopelekea kukosa haki zake za msingi kama mtanzania yeyote anavyostahili.

Ugumu ulioongezeka mnamo Disemba 2019 ulisababisha kuhama kwake kutoka Geita kwenda Mwanza ambako anaishi tangu Disemba 21, 2019.