Mtoto wa jicho
Mtoto wa jicho (kwa Kiingereza: cataract) ni ugonjwa ambao hutokea pale ambapo lenzi ya jicho inakuwa na hali ya uwingu.
Kwa kawaida mitoto ya macho hutokea kwa sababu ya kuzeeka, na uwingu wa lenzi unaweza kupunguza na kuingiza giza katika uoni. Pia inaweza kutokea kwa sababu nyingine, kama majeraha, maradhi ya mwili au ya jicho lenyewe, mnururisho, na kwa nadra hata kwa kuzaliwa nayo.
Kuna aina ya mtoto wa jicho ambayo inaweza kusababisha uoni mfupi (myopia), ambayo inamaanisha huwezi kuona vitu vya mbali lakini unaweza kuona vitu vya karibu.
Ikiwa haitatibiwa kwa upasuaji, baadhi ya aina za mtoto wa jicho zinaweza kusababisha upofu (maana yake huwezi kuona kitu chochote). Ugonjwa huu unaweza kutibika kwa kubadilisha lenzi asili na kuweka nyingine ya plastiki kwa njia ya upasuaji mdogo.
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mtoto wa jicho kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |