Nenda kwa yaliyomo

Mto Liao

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sehemu ya Mto Liao


Mto Liao
Beseni ya mto Liao
Chanzo (vyanzo tofauti tofauti)
Mdomo Hori ya Bohai
Nchi China (majimbo ya Hebei, Mongolia ya Kichina, Jilin, Liaoning)
Urefu km 1,345
Mkondo m3 500
Eneo la beseni km2 232,000

Mto Liao ni mto mkuu kusini mwa eneo la Manchuria nchini China. Liao ni moja kati ya mito mikuu saba ya China. Majina ya majimbo ya Liaoning na rasi ya Liaodong yametokana na mto huo[1]. Mto huo pia unajulikana kama "mto mama" huko kaskazini mashariki mwa China. [2]

Liao inapita kwenye njia yake ya km 1,345 katika beseni lake la kilomita za mraba 232,000.

Hata hivyo inabeba maji kiasi tu maana mkondo wake una m3 500 pekee.

Maji yake huwa na matope mengi maana mto unapita katika ardhi yenye punje ndogo sana kama unga zinazofanya mashapo kuwa mengi.

Njia ya mto

[hariri | hariri chanzo]
Mto Liao kwenye tambarare ya China Kaskazini Mashariki

Mto Liao unaanza mahali pa kuungana kwa matawimto makuu mawili ambayo ni Mto Xiliao (Liao ya magharibi) na Mto Dongliao (Liao ya mashariki).

Mkono wa magharibi wa Liao unapita kabisa ndani ya Mongolia ya Kichina ukiundwa kwa kuungana kwa mito ya Xar Moron na Laoha kwenye sehemu ya 43 ° 25 'N, 120 ° 45' E.

Mkono wa mashariki unaanza katika Jimbo la Jilin, ukipita katika njia yenye umbo la "S" hadi kuungana na mkono wa magharibi.

Sasa Mto Liao wenyewe upo njiani ukielekea kusini kupitia tambarare ya China Kaskazini Mashariki.

Kabla ya kufika baharini mto unajigawa kwa mikono miwili na hivyo kuunda delta yake inayoishia katika bahari ya Bohai.

Matawimto

[hariri | hariri chanzo]

Matawimto makuu

[hariri | hariri chanzo]
  • Mto Xiliao (西辽河, "Mto Liao wa Magharibi") ni tawimto kubwa zaidi la Mto Liao, urefu wake ni km 449 katika beseni dogo la km213,600.
  • Mto Dongliao (东辽河, "Mto wa Liao wa Mashariki") ni chanzo kingine kikuu cha Mto Liao. Ina urefu wa km 360 na beseni dogo la km2 11,500.

Matawimito madogo

[hariri | hariri chanzo]

Mito ifuatayo huingia Mto Liao katika Jimbo la Liaoning.  

  • Mto Sutai ( 苏台河 )
  • Mto wa Qing ( 清河 )
  • Mto Chai ( 柴河 )
  • Shabiki wa Mto ( 泛河 )
  • Mto Xiushui ( 秀水河 )
  • Mto wa Yangximu ( 养息牧河 )
  • Mto wa Liu ( 柳河 )
  • Mto Raoyang ( 绕阳河 )
  1. "Liao River". Encyclopædia Britannica. Iliwekwa mnamo 1 Januari 2013.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Cao, Jie. "Liao River in Deep Trouble" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2009-09-02. Iliwekwa mnamo 1 Januari 2013.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu maeneo ya China bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mto Liao kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.