Nenda kwa yaliyomo

Mto Bell

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mto Bell
Chanzo cha mto Bell
Chanzo Milima ya Drakensberg
Mdomo Mto Orange, kupitia Mto Kraai
Nchi Afrika Kusini
Kimo cha chanzo mita 3,001
Miji mikubwa kando lake Rhodes

Mto Bell ni mto wa Afrika Kusini ambao unapokea maji yake kutoka nyanda za juu za Drakensberg mashariki katika jimbo la Rasi Mashariki. Beseni yake ya utiririshaji inakadiriwa kuwa ni eneo la kilomita za mraba 424 ikianza kwenye kimo cha mita 3,001 juu ya usawa wa bahari na kushuka hadi mita 1720.

Chanzo cha mto kiko karibu na mpaka wa Lesotho  (30°40′34″S 28°08′33″E / 30.67611°S 28.14250°E / -30.67611; 28.14250 (Bell River source)). Kwa kushuka unapitia mji wa Rhodes, hadi kuungana na Mto Sterkspruit na kuanzia hapa yote miwili huitwa Mto Kraai (30°51′08″S 27°46′43″E / 30.85222°S 27.77861°E / -30.85222; 27.77861 (Bell-Sterkspruit confluence)) unaoishia katika Mto Orange (30°40′4″S 26°45′9″E / 30.66778°S 26.75250°E / -30.66778; 26.75250 (Kraai-Orange confluence)).

Mto una idadi kubwa ya samaki aina ya trout. Kila mwaka kuna mashindano ya siku tatu ambako hadi washiriki 80 hushiriki kuvua samaki kwa siku tatu kwenye mwendo wa mto kwa kilomita 180.

Eneo maji yanapokusanyika mlimani lilitumiwa kwa ajili ya shughuli za malisho ya mifugo tangu miaka ya 1870.[1] Hii imesababisha mmomonyoko wa ardhi kwenye ufuko na kuathiri ubora wa maji ya mto Bell.Ili kutatua tatizo hilo  jamii ya mimea ya Salix, hasahasa Salix caprea, zimekuwa zikipandwa pembezoni mwa kingo za mto ili kuzuia mto usije kuhama.[2]

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. Hugo, W.J., 1966, The Small Stock Industry in South Africa, Government Printer, Pretoria.
  2. Rowntree, K.M.; E.S.J. Dollar (1999). "Vegetation controls on channel stability in the Bell River, Eastern Cape, South Africa". Earth Surface Processes and Landforms. 24 (2). Grahamstown: Rhodes University: 127–134. doi:10.1002/(SICI)1096-9837(199902)24:2<127::AID-ESP944>3.0.CO;2-3. ISSN 0197-9337. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2011-07-18. Iliwekwa mnamo 2008-11-23.
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika Kusini bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mto Bell kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.