Msesewe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Msesewe ni kiambato cha pombe chenye ungaunga. Unatokana na mti unaoitwa msesewe.

Utengenezaji[hariri | hariri chanzo]

Wapikaji pombe wanabandua magamba ya msesewe, wanaanika kwenye jua, wanayapigapiga mpaka yawe vipande vidogovidogo, ambavyo hupelekwa mashineni kwa kusaga na kuwa katika hali ya unga.

Utumiaji[hariri | hariri chanzo]

Baada ya pombe kupikwa, unga wa msesewe huongezwa ili kuzidisha ukali wa pombe na pia kuweza kuweka pombe hiyo kukaa kwa muda mrefu. Msesewe hufanya kazi kwa muda wa saa sita tu, pale inapokuwa imepikwa na pombe.

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Msesewe kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.