Nenda kwa yaliyomo

Msamiati (mwanamuziki)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Msamiati

Freddy Benny Mbetwa (anafahamika zaidi kwa jina la kisanii Msamiati) ni msanii na mtunzi wa nyimbo za Hip Hop na Bongo Flava kutoka Tukuyu, Mkoa wa Mbeya, Tanzania.[1]

Tangu aanze muziki, Msamiati ameshafanya kazi na wasanii tofautitofauti wakiwemo Dayoo, Young Lunya, Conboi Cannabino, Country Wizzy, Ben Pol, Mrs Energy na Joh Makini.

Nyimbo zake kama Twende Wote akiwa na Dayoo, Ndagha pamoja na Malafyale akiwa na Young Lunya, zimemfanya kuwa moja ya wasanii bora wa Hip Hop kutoka Tanzania.[2]

Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Msamiati ni mtoto wa kwanza katika familia yake.

Msamiati alianza harakati zake za muziki mwaka 2018 na wimbo wake wa kwanza kufanya vizuri ulikuwa unaitwa Moja Moja ambayo ulitayarishwa na Marco Chali kutokea MJ Records. Wimbo wa Moja Moja ulipokelewa vyema na mashabiki kiasi cha kuchezwa kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM. [3] [4]

Msamiati anajulikana kwa uwezo wake wa kuchanganya lugha ya Kiswahili na Kinyakyusa kwenye muziki wake, kitu ambacho amekionesha kwenye ngoma zake tofauti tofauti kama Unyakyusa Mwingi, Ananichanganya na Malafyale [5]

Wasanii waliomshawishi

[hariri | hariri chanzo]

Mara kwa mara Msamiati amewataja Joh Makini, Albert Mangwair, Solo Thang na Professor Jay kwenye orodha ya wasanii ambao waliathiri na kumshawishi kuingia kwenye tasnia ya muziki. [6]

Nyimbo zake

[hariri | hariri chanzo]
  • Moja Moja (2018)
  • Macho Kodo Ft Ben Pol (2019)
  • Nachana Sana (2019)
  • Ndagha (2019)
  • Yeye (2020)
  • Tununu (2020)
  • Mwaisa (2021)
  • Unyakyusa Mwingi (2021)
  • Wanatoa Mbwa Usiku (2021)
  • Malafyale (2022)
  • Twende Wote (2023)
  • Tumeondoka (2023)
  • Ananichanganya (2023)
  • Bibi Titi (2024)
  1. "How Msamiati is using Nyakyusa-infused Bongo hip-hop to reach global audiences". The Citizen (kwa Kiingereza). 2024-05-09. Iliwekwa mnamo 2024-07-12.
  2. "Msamiati". Music In Africa (kwa Kiingereza). 2020-04-08. Iliwekwa mnamo 2024-07-12.
  3. "Rapa Msamiati Afunguka Jinsi Alivyomvuta Conboi Kwenye "Tumeondoka" ⚜ Latest music news online". mdundo.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-07-12.
  4. Chalz Writes (2024-03-20). "Tanzanian rapper, Msamiati to unveil his own record label". Cityelevens (kwa Kiingereza (Uingereza)). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2024-07-12. Iliwekwa mnamo 2024-07-12.
  5. "Biography: Msamiati's rap recipe is taking Tanzanian Hip Hop to Africa". Latest East African & Bongo Flava Music, Songs & Video - Notjustok (kwa American English). 2024-03-18. Iliwekwa mnamo 2024-07-12.
  6. "Top 10 Bora ya Wanaoibeba Hip Hop TZ". Global Publishers (kwa American English). 2019-10-22. Iliwekwa mnamo 2024-07-12.
Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Msamiati (mwanamuziki) kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.