Nenda kwa yaliyomo

Msaada:Majiranukta

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kuonyesha majiranukta (coordinates) ya mahali juu ya makala

1. Ujipatie majiranukta ya mahali

A) kwa kuitafuta katika makala nyingine ya wikipedia, kwa mfano enwiki
B) kwa kuitafuta kwenye ramani fulani; mfano ufungue ramani za

Ukibofya-kulia kwenye mahhali, unapata chaguo pamoja na kuona majiranukta (Openstreetmaps: "show adress", Google maps "What's here?")

Njia nyingine ni kutafuta katika hazinadata kubwa huko

2. Kutumia kigezo cha desimali

Kama majiranukta zinapatikana kwa umbo la namba mbili za desimali,
mfano A) -10.1590,19.9626 au B) 40.7728,-73.9715,
utatumia kigezo cha A) {{Coord|-10.1590|19.9626|display=title}} au B) {{Coord|40.7728|-73.9715|display=title}}.

Hapa ujue kwamba alama ndogo ya - inasababisha tofauti kubwa! Kama haiko mbele ya namba ya kwanza (latitudo), mahali pataonyeshwa upande wa kaskazini ya ikweta. Tanzania yote na sehemu kubwa ya Kenya iko kusini mwa ikweta, kwa hiyo mahali pao ni lazima kuwa na namba hasi yaani alama ya - mbele ya namba ya kwanza.

Namba ya pili huonyesha nafasi ya longitudo, yaani kama mahali papo upande wa mashariki au magharibi ya mstari unaopita mji wa London-Greenwich (meridiani ya sifuri). Hapa alama ya - inadokeza upande wa magharibi wa London, hivyo nchi zote za Amerika hupata alama hii kwenye nafasi ya pili, pamoja na nchi kadhaa za Afrika ya Magharibi. Sehemu kubwa ya Afrika na Ulaya, pamoja Asia yote una onyesha namba chanjo yani bila alama ya - mbele ya namba ya pili.


3. Kutumia kigezo cha nyuzi

Wakati mwingine utakuta majiranukta kwa umbo 57°18′22″N 4°27′32″W. Umbo hilo huunyesha majiranukta kwa kutaja nyuzi, dakika na sekunde za tao.

Pia hapa sehemu ya kwanza huonyesha latitudo (kaskazini-kusini) na sehemu ya pili huonyesha longitudo (mashariki-magharibi). Kila sehemu hugawiwa kwa nyuzi, dakika na sekunde za tao.

Hapa tunatumia kigezo cha {{Coord|57|18|22|N|4|27|32|W|display=title}}. Ni lazima kutaja kaskazini/kusini kwa herufi za N au S, halafu mashariki/magharibi kwa herufi za E au W.

Msimbo wa "title" inaonyesha majiranukta juu ya matini yote kwenye nafasi ya kwanza ya makala.

4. Muonekano upande wa kulia au katikati

Ukitaka majiranukta yaonekane kwenye kona ya juu upande wa kulia. unaweze kutumia amri

<div style="text-align: right;"> {{Coord|-12.3456|12.3456|display=title}} </div> .

Ukitaka ionekane katikati, tumia center badala ya right.