Nenda kwa yaliyomo

Mr Joel Joseph

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Joel Vicent Joseph
Faili:Mrpuaz.jpg
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Joel Vicent Joseph
Amezaliwa 31 Machi 1985 (1985-03-31) (umri 39)
Aina ya muziki Bongo Flava
Kazi yake Meneja Wa Talanta
Miaka ya kazi 2002 mpaka Sasa
Tovuti http://www.instagram.com/mrjoelvjoseph

Joel Vicent Joseph (anajulikana kama Mr Joel Joseph[1]; alizaliwa Arusha, Tanzania, 31 Machi 1985) ni Mwigizaji, Mwandishi, Mwanamuziki na Meneja wa talanta[2][3], kutoka Tanzania. Mr Joel Joseph alisainiwa chini ya studio ya rekodi iitwayo WCB Wasafi ili kumsimamia Harmonize.[4][5][6].

Maisha ya awali na elimu

[hariri | hariri chanzo]

Joel amezaliwa jijini Arusha, Tanzania tarehe 31 Machi 1985, mahali wazazi wake wamekulia na kuishi. Alihitimu masomo yake ya sekondari mwaka 2005 Marangu Secondary School alienda katika chuo cha uhandisi wa kompyuta kiitwacho New Horizon Institute na kupata shahada yake ya kompyuta. Baadae aliendeleza masomo yake kwa kuchuku kozi mbali mbali kwa kutumia elimu ya mtandaoni ( E- Learning ) na kujichukulia vyeti vya kozi mbali mbali ikiwemo Usimamizi wa Ajira kutoka Harvards Business Publishing.

Maisha ya Kimuziki

[hariri | hariri chanzo]

Mr Joel Joseph[7] alianza muziki akiwa na miaka 21, Alikuwa akijihusisha na kuimba nyimbo za wasanii wengine (Cover Songs) ambapo ilimpelekea kujua kwamba ana uwezo wa kuimba hivyo kutunga nyimbo zake mwenyewe. Mnamo mwaka 2005, Mr. Joel Joseph aliingia kurekodi wimbo wake wa kwanza uitwao SWEET BABY, uliorekodiwa chini ya studio za Grandmaster Records zilizopo jijini Arusha,Tanzania. 2006 alishiriki kutoa wimbo mwingine akiwa katika kundi akitumia jina Nizzo B[8]. Wimbo huo unaitwa "USIKU WA LEO" kazi ambayo imefanya vizuri kwenye Purebreak Chart kubwa za Ufaransa.

Kazi yake ya meneja wa talanta

[hariri | hariri chanzo]

Mnamo mwaka 2018 Mr.Joel Joseph alisainiwa chini ya usimamizi wa studio rekodi iitwayo WCB Wasafi kwa ajili ya kumsimamia mwanamuziki Harmonize katika kazi zake. Moja kati ya mafanikio ya kazi kubwa alizofanya ni kumjenga Harmonize na kuikuza sanaa yake ya muziki. katika kazi zilizoleta mafanikio makubwa moja wapo ilikuwa ni "kwangwaru" ambayo ni kazi ilibadilisha maisha ya mwanamuziki Harmonize kwa upande mkubwa,na hii ilimpa nafasi kubwa sana ya kuwa mmoja wa mameneja hodari wa Talanta Tanzania. kuacha "kwangwaru"" Mr Joel Joseph amezisimamia kazi nyingine zikiwemo "Dm Chick" iliyomshirikisha mwanamuziki wa Ghana "Sarkdie", Atarudi pamoja na Kadamshi. " Kwangwaru iliwezakuchukua nafasi mbali mbali na kushiriki katika tuzo mbali mbali Afrika ikiwemo African Muzik Awards (AFRIMMA). Licha ya kuwafanya kazi na Harmonize , pia Mr Joel ameshawahikufanya kazi na msanii Shetta akiwa kama meneja wake.[8] Mwaka 2018 mwishoni Mr Joel alitangaza rasmi kuacha kufanya kazi Wasafi Classic Baby (WCB) na kuacha kufanya kazi na msanii Harmonize.[9] Kwa mujibu wa BBC[2] ilieleza kuwa Mr puaz alitengana na mwanamuziki huyo kwa sababu ya kutofautiana katika mazingira ya kazi na vile vile kauli.

Mwaka Jina Mchapaji ISBN
2023 Mwenendo Wa Biashara Ya Muziki Barani Afrika) Pencil Publishers ISBN 978-93-56676-61-9
Mwaka Filamu Wadhifa
2018 10X10 Mwigizaji na Mwongozaji
2009 A Grain Of Sand Mwigizaji
2008 Bongo Land II: There Is No Place Like Home Mwigizaji
1991 The History & Usage Of Khanga In East Africa Mwigizaji
Jina la wimbo Mwaka
"Sweet Baby" 2004
"Usiku wa leo" 2015 "Party la leo" 2023
  1. "Mr Joel Joseph Biography". Music In Africa (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2018-07-04.
  2. 2.0 2.1 Hamornize atengana na meneja wake (kwa Kiingereza (Uingereza)), 2019-01-03, iliwekwa mnamo 2019-01-21
  3. "Mr Puaz Biography, Songs & Albums". AMDb (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-09-22. Iliwekwa mnamo 2019-01-24.
  4. "Meet the man tasked to handle Harmonize by Diamond (Photos)". Facebook (kwa American English). 2018-05-08. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-04-19. Iliwekwa mnamo 2019-03-05.
  5. Watiri, Sue, Meet the man tasked to handle Harmonize by Diamond (Photos) (kwa American English), ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-06-29, iliwekwa mnamo 2018-07-04
  6. "ONE ON ONE: Harmonize", Daily Nation (kwa Kiingereza), iliwekwa mnamo 2018-07-04
  7. "Tanzanian singer 'to publish music business book'". Music In Africa (kwa Kiingereza). 2018-08-09. Iliwekwa mnamo 2019-01-24.
  8. 8.0 8.1 Steve Biko (2019-02-09). "Mr Puaz". Afro Muziki (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-02-24. Iliwekwa mnamo 2019-03-05.
  9. Queen Serem (2019-01-04). "EXCLUSIVE: Harmonize's manager Mr Puaz exits WCB". Mpasho News (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2019-03-05.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mr Joel Joseph kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.