Mr Eazi
Mr Eazi | |
---|---|
| |
Jina Kamili | Oluwatosin Ajibade |
Jina la kisanii | Mr Eazi |
Nchi | Nigeria |
Alizaliwa | 19 Julai 1991 |
Aina ya muziki | Afropop, Rap |
Kazi yake | Mwanamuziki |
Miaka ya kazi | 2012 - hadi leo |
Kampuni | Banku Music |
Oluwatosin Ajibade (aliyezaliwa 19 Julai 1991), anayejulikana zaidi kwa jina lake la kisanii Mr Eazi, ni mzaliwa wa Nigeria, mwimbaji anayeishi Ghana.[1] Yeye ni mwanzilishi wa muziki wa Banku.[2] Bw Eazi alihamia Kumasi, Ghana mwaka wa 2008 na kujiandikisha katika chuo cha Kwame Nkrumah University of Science and Technology (Kifupi: KNUST), ambapo alianza kuweka nafasi za wasanii kutumbuiza kwenye karamu za chuo kikuu. Alionyesha kupendezwa na muziki baada ya kurekodi wimbo wa kushirikishwa wa "My Life", wimbo ambao ulipata mvuto na kuwa rekodi maarufu chuoni apo. Mr Eazi alitoa mixtape yake ya kwanza ya "About to Blow" mwaka wa 2013. Alipata hadhi ya kimataifa kufuatia kutolewa kwa wimbo aliosaidiwa na Efya "Skin Tight". Mixtape yake ya pili ya Life Is Eazi, Vol. 1 - Accra To Lagos ilitolewa mnamo 2017.
Maisha na elimu
[hariri | hariri chanzo]Mr Eazi alizaliwa Port Harcourt, mji mkuu na jiji kubwa zaidi katika Jimbo la Rivers, Nigeria. Alikulia katika familia ya ujasiriamali. Mama yake alikuwa ni mfanyabiashara ndogo ndogo na baba yake ni rubani.[3] Akiwa anahudhuria shule ya msingi mjini Lagos, Mr Eazi alikuwa na muda mfupi katika kwaya ya shuleni apo. Wakati wa malezi yake, alisikiliza sana rekodi ambazo baba yake alipendelea kusikiliza wakati wa kupata kifungua kinywa. Akiwa na umri wa miaka 16, Mr Eazi alihamia nchini Ghana kuendeleza shughuli zake za elimu, na alijiandikisha katika programu ya uhandisi wa mitambo katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Kwame Nkrumah (KNUST). Mr Eazi alianza kurekodi muziki wakati alipokuwa KNUST. Alichangia sauti kwenye wimbo wakushirikishwa wa "My Life", wimbo ambao ulipata mvuto na kuwa rekodi maarufu katika chuo cha KNUST. Kabla ya hapo, alianzisha kampuni ya matangazo iitwayo Swagger Entertainment. Alitumia jukwaa hilo kuandaa maonyesho na kutangaza matukio katika chuo kikuu cha KNUST.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Mr Eazi: Biography, Age, Education, Girlfriend, Songs, Net worth, and Source of wealth". News Wirengr (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-06-19.
- ↑ "Introducing Mr Eazi, the OVO and Wizkid Favorite Bringing Afrobeats to the Masses". Complex (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-02-13. Iliwekwa mnamo 2017-02-13.
- ↑ "Mr. Eazi Wants to Connect a Billion People Through Afrobeats". Vice (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2017-04-15.
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mr Eazi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |