Nenda kwa yaliyomo

Mount Rushmore

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sanamu kwenye Mount Rushmore ni vichwa vya George Washington, Thomas Jefferson, Theodore Roosevelt Abraham Lincoln ((kuanzia upande wa kushoto)
Mlima Mount Rushmore kwa jumla

Mount Rushmore ni mlima mashuhuri nchini Marekani uliopo kwenye safu la milima ya Black Hills katika jimbo la South Dakota.

Mount Rushmore imekuwa mashuhuri kwa sababu pana sanamu za marais manne wa Marekani George Washington, Thomas Jefferson, Theodore Roosevelt na Abraham Lincoln. Kila kichwa kina kimo cha mita 18. Msanii Gutzon Borglum alichonga mawe magumu ya matale kati ya 1927 hadi 1941 kwa msaada wa wafanyakazi 400 akitumia baruti pamoja na mashine za kuchonga.

Maindio wa Lakota ambao ni wenyeji asilia wamesikitishwa na sanamu hizi kwa sababu kwao milima ya Black Hills ni mahali patakatifu.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya Marekani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mount Rushmore kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Wikimedia Commons ina media kuhusu: