Monica Bellucci

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Monica Bellucci
Monica Bellucci
Monica Bellucci
Jina la kuzaliwa Monica Anna Maria Bellucci
Alizaliwa 30 Septemba 1964, Città di Castello, Umbria, Italia
Kazi yake Mwigizaji
Mwanamitindo
Ndoa Vincent Cassel (1999-hadi leo)

Monica Anna Maria Bellucci (amezaliwa tar. 30 Septemba 1964) ni mwigizaji na mwanamitindo kutoka nchini Italia.

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Maisha ya awali[hariri | hariri chanzo]

Bellucci alizaliwa mjini Città di Castello, Umbria, Italia, akiwa kama binti wa Maria Gustinelli, mchoraji, na Luigi Bellucci, ambaye anamiliki kampuni ya magari makubwa ya kusafirishia mizigo.

Bellucci alianza shughuli za uwanamitindo tangu yungali na umri wa miaka 16, pale alipohitimu elimu yake ya sekondari katika shule ya Liceo Classico.

Hapo awali alijifua na elimu ya uwanasheria, lakini kwa uwanamitindo wake ulimsaidia kujipatia vijisenti vya kumwendeleza kwa masomo ya twisheni wakati akiwa anasoma katika Chuo Kikuu cha Perugia, na maisha ya urembo yalimfanya Monica kuwa mbali na masomo yake ya uwanasheria.

Belluci ni mzungumzaji mzuri wa lugha ya Kitaliano, Kifaransa na Kiingereza kwa ufasaha - vilevile Kihispania, na pia amewahi kucheza filamu nyingi tu kwa lugha hizo.

Filamu alizocheza[hariri | hariri chanzo]

 • Bram Stoker's Dracula (1992)
 • L'appartement (1996)
 • Dobermann (1997), Nat the Gypsy
 • Under Suspicion (2000)
 • Malèna (2000)
 • Le Pacte des Loups (2001)
 • Astérix & Obélix: Mission Cléopâtre (2002)
 • Irréversible (2002)
 • Tears of the Sun (2003)
 • Ricordati di me (2003)
 • The Matrix Reloaded (2003)
 • The Matrix Revolutions (2003)
 • The Passion of the Christ (2004)
 • She Hate Me (2004)
 • The Brothers Grimm (2005)
 • Manuale d'amore 2 - Capitoli successivi (2006)
 • Shoot 'Em Up (2007)
 • Heart Tango (2007)

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons