Mongomongo
Mongomongo ni kijiji kilichopo mashariki mwa Wilaya ya Lindi Vijijini, kilometa 17.08 kutoka Lindi mjini.Katika sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 kijiji kilikua na jumla ya idaidi ya watu 561. Ikiwa ni 268 wanaume na 293 ni wanawake,kijiji kina urefu wa mita za mraba 805.91 na upana wa mita za mraba 398.25.
Kijiji cha Mongomongo kina jumla ya vitongoji vinne navyo ni; Mongomongo, Mtohutohu, Mang’ang’a na Pwani. Kuna umbali wa kilomita 4.75 kutoka kwenye kitongoji cha mongomongo hadi kitongoji cha pwani, na kilomita 2.75 kutoka kitongoji cha mongomongo hadi kitongoji cha mang’ang’a.
Kijiji cha Mongomongo kimepakana na kijiji cha Navanga kwa upande wa kusini magharibi, na umbali wa kilomita 6.19 kutoka Mongomongo hadi Navanga, kwa upande wa kusini Mongomongo imepakana na kijiji cha Nachunyu, na umbali wa kilomita 9.32 kutoka Mongomongo hadi Nachunyu, na upande wa kusini mashariki Mongomongo imepakana na kijiji cha Lideko, na umbali wa kilomita 6.17 kutoka Mongomongo hadi Lideko, na upande wa kaskazini mashariki Mongomongo imepakana na kijiji cha Shuka,kilomita 6.03 kutoka Mongomongo hadi Shuka,na upande wa mashariki Mongomongo imepakana na Bahari ya Hindi kwa umbali wa kilomita 4.75.
Wakazi wa kijiji cha Mongomongo wanajishughulisha na shughuli za kilimo, uvuvi, ufugaji na biashara ndogondogo kama vyanzo vyao vya kipato, na mazao yanayo limwa katika kijiji cha Mongomongo ni korosho,ufuta na karanga kama mazao makuu ya biashara na mtama,mahindi,na muhogo kama mazao ya chakula. Pia pamoja na hayo kuna baadhi ya wanakijiji wanajihusisha na uwindaji wa wanyama pori.
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Lindi bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mongomongo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |