Mnyama-upupu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mnyama-upupu
Konyeza sahihi (Chrysaora fuscescens)
Konyeza sahihi (Chrysaora fuscescens)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia
Nusuhimaya: Eumetazoa
Faila: Cnidaria
Hatschek, 1888
Ngazi za chini

Nusufaila na ngeli:

Umbo wa wanyama-upupu; nyekundu: exodermi; kijivu: mesoglea; buluu: gasterodermi; samawati: uwazi wa mmeng'enyo
Mzunguko wa maisha wa konyeza

Wanyama-upupu (kutoka Kiholanzi neteldier) ni wanyama sahili wa bahari au maji baridi ambao wana seli zinazochoma ngozi na zinazoweza kukamata samaki na wanyama wadogo wengine. Anthozoa kama matumbawe wamekazika chini lakini takriban wote wa Medusozoa huogelea majini. Spishi chache kiasi tu zinatokea majini baridi.

Mwili wa wanyama-upupu umeumbwa kwa tabaka la kolajini (collagen) na proteoglycans lililofunikwa na seli nje na ndani. Tabaka la nje la seli liitwa exodermi (exoderm) na tabaka la ndani liitwa gasterodermi (gastroderm). Kati ya mwili ni uwazi wa mmeng'enyo ulio na kipenyo kimoja kilikopo juu katika Anthozao na chini katika Medusozoa. Anthozoa wana minyiri mifupi kiasi kuzunguka kipenyo hiki, lakini minyiri ya konyeza ni mirefu.

Picha[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu "Mnyama-upupu" inatumia neno (au maneno) ambalo si kawaida na matumizi yake ni jaribio la kutafsiri neno (au maneno) la asili neteldier kutoka lugha ya Kiholanzi. Neno (au maneno) la jaribio ni mnyama-upupu.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala.

Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.