Mlinzi Mkuu wa Mwalimu Nyerere

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mlinzi Mkuu wa Mwalimu Nyerere ni kitabu kilichoandikwa na Peter Bwimbo aliyekuwa mlinzi mkuu wa Mwalimu Julius Nyerere katika kipindi cha kabla ya uhuru na baada ya uhuru [1]

Kitabu hiki kimetoka kwa mara ya kwanza mwaka wa 2016, kikiwa kinaelezea wasifu wa aliyekuwa mlinzi mkuu wa kwanza wa Baba wa taifa la Tanzania, historia yake kuhusu maisha yake binafsi na maisha ya utumishi kama Bodyguard mkuu wa Kikosi cha ulinzi cha raisi.

Ni kitabu kilichobeba historia ya taifa la Tanzania kikitazama hali iliyokuwepo kabla na baada ya uhuru katika idara za polisi na jinsi ambavyo yeye na wenzake waliweza kushirikiana katika kuhakikisha rais anakuwa salama muda wote.

Katika kitabu hiki mwandishi amejitahidi kuelezea changamoto ambazo walikuwa wanapitia kama walinzi wa rais huku changamoto mojawapo ikiwa ni ile ya kumtoa rais ikulu wakati wa maasi ya Tanganyika Rifles [2] na namna alivyoweza kufanikisha kuifanya Oparesheni magogoni na kumtoa rais ikulu kabla ya wanajeshi kufika ikulu.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. D.M, Bwimbo, Peter (2015-11-03). Peter DM Bwimbo: Mlinzi Mkuu wa Mwalimu Nyerere (kwa Kiswahili). Mkuki na Nyota Publishers. ISBN 978-9987-753-32-1. 
  2. "MIAKA 20 BILA NYERERE: Nyerere apata msukosuko-5". Mwananchi (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2020-02-02. 
Makala hii kuhusu kitabu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mlinzi Mkuu wa Mwalimu Nyerere kama Mwandishi wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.