Mlima Abuna Yosef

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mlima Abuna Yosef iliopo nchiniEthiopi

Abuna Yosef ni mlima maarufu ulio karibu na mwinuko wa mashariki wa Nyanda za Juu za Ethiopia. Una urefu wa mita 4,260 (futi 13,976) juu ya usawa wa bahari. Ni mlima wa sita kwa urefu nchini Ethiopia na mlima wa 19 kwa urefu barani Afrika. Unapatikana sehemu inayojulikana kama Lasta Massif katika eneo la Semien Wollo, Mkoa wa Amhara.

Kitu kinachojulikana sana kwenye mlima huo ni Kanisa la Gennete Maryam, kanisa lililochongwa mwambani ambalo liliripotiwa kuwa kanisa la mila lilifutwa wakati wa utawala wa Yekuno Amlak. [1]

Pia makanisa manne yaliyokuwa yakijitegemea yalijengwa ndani ya mapango ya mlima, kanisa kongwe na maarufu zaidi lilikuwa ni Kanisa la Yemrehana Krestos, lililojengwa na mfalme wa Zagwe (Mfalme wa jina moja). Matatu mengine ni Emakina Medhane Alem (linakisiwa huenda lilijengwa na Yekuno Amlak mwishoni mwa karne ya 13), Lidetta Maryam na Zammadu Maryam (nayo yanakisiwa huenda yalijengwa karne ya 15). [2] Makanisa ya Lalibela yapo katika sehemu za chini za milima.

Sehemu ya Uhifadhi wa mlima huu hupatikana Jamii ya Abuna Yosef inajumuisha kilomita za mraba 70 za ngome ya Abuna Yosef. [3]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Philip Briggs, Ethiopia: The Bradt Travel Guide, 5th edition (Chalfont St Peters: Bradt, 2009), p. 368
  2. Gervers, Michael. "An Architectural Survey of the Church of Emakina Madhane Alam (Lasta, Ethiopia)". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-01-14. Iliwekwa mnamo 17 March 2014.  Check date values in: |accessdate= (help)
  3. http://www.ethiopianwolf.org/publications/EWCP-Annual-Report-April-2013.pdf Archived 7 Septemba 2014 at the Wayback Machine. Annual report. Ethiopian Wolf Conservation Programme. 2013. p. 9. Retrieved 24 May 2014.
Makala hii kuhusu maeneo ya Ethiopia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mlima Abuna Yosef kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.