Mlango wa mashua

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mlango wa mashua na meli ndogo kwenye Mto Neckar, Ujerumani

Mlango wa mashua (Kiing. lock) ni kifaa kinachoruhusu kupandisha au kushusha mashua, boti au meli kati ya mito na mifereji yenye usawa tofauti wa maji. Sehemu kuu ya mlango wa mashua ni chemba cha maji ambacho wa kawaida huwa na geti mbili; moja upande wa usawa wa juu wa maji na nyingine upande wa usawa wa chini wa maji.Chumba huwa na urefu unarohusu mashua au meli kuingia wakati geti zote zinafungwa.

Katuni inayoonyesha kazi ya mlango wa mashua
Milango ya Neptune's Staircase kwenye Mfereji wa Kaledonia, Uskoti

Mahali pa milango ya mashua[hariri | hariri chanzo]

Milango ya mashua inahitajika

  • kama mto unabadilisha usawa wake kwa umbali mdogo, kwa mfano penye maporomoko
  • pale ambako mfereji unajengwa kwenye nchi penye usawa tofauti kama miinuko na mabonde; milango inaruhusu mfereji pamoja na mashua "kupanda mlima" na "kushuka mlima".
  • pale ambako mfereji unaunganishwa na mto mwenye usawa wa maji tofauti, au pale ambako mifereji miwili inakutana.

Kazi ya mlango wa mashua[hariri | hariri chanzo]

Usawa wa maji ndani ya chemba hubadilishwa hadi inalingana na upande ambao mashua inaelekea. Mabadiliko hayo hutekelezwa ama kwa kufungua geti upande wa maji juu na hivyo chemba chote kinajaa sawa na usawa wa juu. Hapa mashua kutoka upande wa juu inaweza kuingia na geti ya juu inafungwa.

Sasa geti ya chini inafunguliwa kidogo na maji hutoka hadi kufikia usawa wa upande wa chini. Mara usawa huo wa chini umefikiwa, geti ya pili inafunguliwa kabisa na mashua inaweza kuondoka upande wa usawa chini.

Wakati mashua inahitaji kupanda, maji ndani ya chemba inatolewa kwa kufungua geti upande wa chini. Mara usawa ndani ya chemba unalingana na sehemu ya chini, mashua inaingia na geti inafungwa. Sasa maji huingizwa kutoka upande wa juu na chemba kinajaa maji hadi kufikia usawa wa juu. Sasa geti ya juu inafunguliwa na mashua inaweza kuendelea upande wa juu.

Milango ya ngazi[hariri | hariri chanzo]

Mifereji wakati mwngine huwa na mfululizo wa milango inayofuatana kama sehemu za ngazi. Zinapatikana hasa kwenye milango ya zamani iliyoendeshwa kwa nguvu ya mkono.

Siku hizi milango ya kisasa huendeshwa kwa nguvu ya mashine ina uwezo wa kushusha maji ndani ya chemba kimoja mita nyingi zaidi.

Kazi ya mlango wa mashua kwenye mfereji

1-3. Boti inaingia mlango ukiwa na usawa wa chini

4. Geti za chini zinafungwa, geti za juu kufunguliwa, chemba kuanza kujaza

5. Mlango unajaa maji, kuinua mashua hadi usawa wa juu

Marejeo[hariri | hariri chanzo]